Mkurugenzi wa
St. Merry School
na New Palm Hotel iliyopo Bagamoyo, Ndugu Mutta Rwakatale kesho ijumaa,
saa 6.30 Mchana katika ofisi za Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) zilizopo
karibu na uwanja wa ndani wa Taifa (indoor stadium) atatoa vifaa vya mazoezi na nauli kwa
wachezaji wa timu ya taifa inayofanya mazoezi uwanja wa taifa wa ndani kwa
ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa, tukianzia
kushiriki mashindano ya ubingwa wa
Afrika yatakayofanyika kuanzia Sept. 01-07/2013 nchini Mauritius, Mashindano ya
Jumuiya ya Madola 2014, Mashindano ya Afrika 2015 Mashindano ya Olimpiki 2016
na mengine mengi.
BFT tumefurahishwa mno na mwitikio wa Mkurugenzi huyo
kwa kusikia na kuguswa kuhusu timu ya taifa ya ngumi na BFT tunaona msaada huo umekuja kwa muda mwafaka kwa kuwa
timu yetu ya taifa inafanya mazoezi
katika hali duni, kwa kutumia vifaa ambavyo
vimechakaa, lakini pia wachezaji walikuwa wanafika mazoezini kwa
kujitolea wao kama wao kwa nauli zao, hivyo tunaamini msaada huo utaleta hamasa
zaidi kwa wachezaji kipindi hiki kilichobakia kabla ya kwenda kushiriki
mashindano ya ubingwa wa Afrika nchini Mauritius, kwani tunaamini sasa ratiba
ya makocha itafanyika kama walivyopanga na wachezaji wataweza kufika wote
mazoezini na kwa wakati.
BFT tunawaomba watanzania wengine wajitokeze zaidi
kusaidia timu yetu ya taifa ili uwakilishi katika mashindano ya kimatifa uwe
wenye tija.kwa kuzingatia kuwa watanzania wote ndio wanachohitaji na ili
kitimie mabondia lazima tuwaandae vema.
Pia naomba sana
vyombo mbalimbali vya habari kujitokeza katika hafla hiyo fupi kwa nia ya
kuhamasisha ili watanzania wengine kujitokeza kuendelea kusaida zaidi maana
bado msaada unahitajika wa vifaa vya mazoezi, matibabu, chakula, maji,nauli,
nguo za mazoezi na posho