1. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa
Tanzania Premier League Board utafanyika tarehe
18 Oktoba 2013 jijini Dar es salaam. Wajumbe wa Baraza la TPL Board
wanaopenda kuwania nafasi za uongozi wa TPL Board wanataarifiwa kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TPL Board
zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe 20 Agosti 2013 katika
Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF ( Idara ya
Fedha), kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa
kurudisha Fomu ni saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti, 2013.
2. Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni hizi zifuatazo:
(i)
Mwenyekiti
wa TPL Board.
(ii)
Makamu Mwenyekiti wa TPL Board.
(iii)
Wajumbe wawakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board (TPL Board
Management Committee), nafasi mbili (2).
3.
Mtu yeyote
anayeomba nafasi ya uongozi katika TPL Board lazima atimize masharti
yafuatayo:
(i)
Awe Raia wa Tanzania
(ii)
Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha
Nne na cheti cha kuhitimu elimu ya Sekondari.
(iii)
Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu
uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)
Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na
kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)
Awe na umri wa angalau miaka 21.
(vi)
Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu,
Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya
Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(vii)
Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa
TPL Board awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya
sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu uliopita (2012/13).
(viii)
Kwa nafasi za
Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya
Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu Daraja la Kwanza .
4.
Ada za Fomu za maombi ya
uongozi ni hizi zifuatazo:
(i)
Mwenyekiti
na Makamu Mwenyekiti wa TPL
Board; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
(ii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPL Board;
Shillingi Laki moja (Tshs. 100,000/=).
5.Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika
mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile
walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa
kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili
kuthibitisha malipo yao.
6. Ratiba ya mchakato wa Uchaguzi wa TPL Board
imeainishwa hapa chini:
Na.
|
TAREHE
|
SHUGHULI
|
1.
|
14/08/2013
|
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kutangaza Uchaguzi wa TPL Board, nafasi za kugombea na sifa za kugombea
uongozi wa TPL Board.
|
2.
|
16/08
/2013 – 20/08/2013
|
Kuchukua Fomu za maombi ya
uongozi wa TPL Board kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Katibu
Mkuu wa TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 10.00
Alasiri. Mwisho wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF ni Jumanne tarehe
20/08/2013 saa 10:00 Alasiri.
|
3.
|
21-23
/08/2013
|
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kupitia fomu za waombaji uongozi wa TPL Board. Kutangaza matokeo ya upitiaji
fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa
TPL Board (23/08/2013).
|
4.
|
24/08/2013-26/8/2013
|
Kutoa fursa ya pingamizi kwa
waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 26/08/2013 saa 10:00
Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie
matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za Uchaguzi.
|
5.
|
27/8/2013-
29/08/2013
|
Wawekaji Pingamizi na
waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa utetezi
wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi
|
6.
|
30/08/2013
- 03/09/2013
|
. Usaili na kutangaza matokeo
ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya
usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea
|
7.
|
04
– 06/09/2013
|
Kamati ya Uchaguzi kupitia
Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote
ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF.
|
8.
|
04
– 06/09/2013
|
Kutoa fursa ya kukata Rufaa
kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF Elections Appeal Committee)
kwa masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya
Rufaa zitapokelewa na Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe
06/09/2013 saa 10:00 Alasiri.
|
9.
|
07-13/09/2013
|
Kamati ya Maadili ya TFF
kupitia mashauri yote yanayohusu
Maadili na kuyatolea uamuzi.
|
10.
|
14-
16/09/2013
|
Kamati ya Maadili ya TFF
kutoa matokeo ya maamuzi ya mashauri ya maadili kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF
na wagombea.
|
11.
|
17-
19/09/2013
|
Kukata Rufaa kwenye Kamati ya
Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 19/09/2013 saa
10:00 Alasiri
|
12.
|
20-
24/09/2013
|
Kusikiliza Rufaa
zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF na kutolea uamuzi.
|
13.
|
25-27
/09/2013
|
Kamati ya Rufaa ya Maadili ya
TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea matokeo ya Rufaa
zilizosikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili
|
14.
|
28/9/2013
– 2/10/2012
|
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi
kusikiliza rufaa za uchaguzi wa TPL Board kwa masuala yasiyo ya Maadili.
|
15.
|
03-04/10/2013
|
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi
ya TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya rufaa wagombea waliokata
rufaa (zisizohusu mashauri ya Maadili).
Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa
hizo.
|
16.
|
05/10/2013
|
Kutoa orodha ya wagombea wote
waliopitishwa kugombea uongozi wa TPL Board na kuwataarifu wajumbe wa Baraza
la TPL Board.
|
17.
|
06/10/2013-17/10/2013
|
Kipindi cha kampeni kwa wagombea wote
|
18.
|
18/10/2013
|
Uchaguzi wa viongozi wa TPL
Board
|
7.
Uchaguzi wa TPL Board unafanyika kwa mujibu wa
Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF.
Hamidu Mbwezeleni
MWENYEKITI
KAMATI
YA UCHAGUZI YA TFF