Ratiba ya michuano ya U15 Copa Coca-Cola ngazi ya
Ratiba ya
michuano ya U15 Copa Coca-Cola ngazi ya kanda mwaka huu itapangwa keshokutwa
(Agosti 29 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Michuano
hiyo ya kanda itaanza Septemba Mosi mwaka huu wakati mikoa inakumbushwa kuwa
inatakiwa iwe imewasilisha usajili wa wachezaji wao kufikia Agosti 28 mwaka huu
kupitia email ya TFF ambayo ni tanfootball@tff.or.tz na nakala kwa
madadi_salum@ yahoo.com
Pia mikoa
inakumbushwa kutowajumuisha wanafunzi wa darasa la saba katika timu zao katika
ngazi ya kanda na fainali itakayochezwa Dar es Salaam kuanzia Septemba 7 mwaka
huu kwa vile watakuwa katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi. Timu
zinatakiwa kufika vituoni Agosti 30 mwaka huu.
Kanda hizo
ni Mwanza itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida
inaunda Kanda ya Arusha.
Zanzibar
itakuwa na Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja wakati Kanda
ya Dar es Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke na mkoa mmoja wa
Unguja.
Kanda ya
Mbeya inaundwa na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma wakati Dodoma,
Morogoro, Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.
Mwanza
itatoa timu nne kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za Arusha timu
mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza timu mbili.