Na Dina
Ismail
SIMBA imejikuta ikihaha kupigania mabao matatu na pointi
tatu ilizopokwa na kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Vinara hao
wa ligi kuu walikata rufaa kwa kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi
Tanzania ‘kamati ya masaa 72’ ikidai Kagera Sugar kumchezesha beki mohammed
Fakhi wa Kagera Sugar wakati akiwa ana
kadi tatu za njano.
Katika
mchezo huo uliopigwa katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba Aprili 2 mwaka huu, Simba ililala kwa mabao
2-1.
Kwamba,
kamati ya masaa 72 iliipa mabao matatu na pointi tatu Simba baada ya kujiridhisha kwamba Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.
Hata hivyo
Kagera Sugar ilipinga na kukimbilia kamati ya katiba Sheria na Hadhi
wachezaji kabla ya kamati hiyo kuamua
kuipoka ushindi huo wa mezani Simba baada ya kugundua kuwepo kwa makosa kadhaa
katika kuipa ushindi wa mezani Simba.
Selestine
Mwesigwa, Katibu Mkuu wa TFF akizungumzia hatua hiyo alibainisha mambo kadhaa
yaliyopelekea kubatilishwa kwa maamuzi hayo ikiwemo Simba kutowasilisha kwa
wakati na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 20 kifungu cha kwanza cha kwanza cha
kanuni za Ligi Kuu toleo la mwaka 2006 inayotaka malalamiko yote yawasilishwe
kwa maandishi Bodi ya Ligi siyo zaidi ya saa 72 baada ya mchezo kumalizika kwa
mchezo.
Pili,
Mwesiga alisema malalamiko hayo
hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni ya 20 kifungu cha nne kinachosema ada ya
malalamiko ni Sh. 300,000 na kwamba malalamiko yatakayowasilishwa bila kulipiwa
ada au baada ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.
Sababu ya
tatu aliyoitaja Mwesigwa ni kwamba kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji
wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali baada ya
kuwashirikisha Wajumbe waalikwa ambao siyo sehemu ya Kamati hiyo.
Maamuzi hayo
yameonekana kuichanganya sana Simba na hivyo kuwa na mikakati ya kuhakikisha
inapanda ngazi za juu zaidi ili kuweza kudai haki yao.
Nadhani
Simba ingeachana na hili suala na kuelekeza nguvu zake katika michezo yake ya
Luigi ambayo imebakiza wiki chache kabla ya kumalizika.
Kwamba,
inawezekana ni kweli wana haki lakini walifanya makosa wenyewe katika hatua za
awali za kukata kwao rufaa kwa kukosea baadhi ya kanuni na taratibu zilizopo
katika katika ya TFF kama kama alivyoeleza Katibu Mkuu wa TFF
Hivyo basi
kuendelea kufuatilia suala hilio ni kupoteza muda kwani nguvu inayotumika
katika zoezi hilo ni bora ingeelekezwa katika maandalizi ya michezo iliyonayo
timu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza Ligi hiyo
ikiwa na pointi 59, huku mabingwa watetezi Yanga wakishika nafasi ya
pili kwa pointi 56.
Sote
tunafahamu Simba imepania kutwaa ubingwa wa Bara msimu wa 2016/2017 baada ya
kuukosa kwa miaka zaidi ya mitano hivyo ni vema ikajiongeza kwa kupata ushindi wa
halali badala ya kubaki inaililia pointi za bure.