Na Dina
Ismail
KUNA
usemi maarufu ‘Mdharau mwiba, mguu huota
tende!
Huu msemo
una maana kubwa sana na ni wajibu kuutilia maanani.
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga Sc kwa leo ndio walengwa wa msemo huu.
Kwa miezi
kadhaa sasa hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya
jangwani na Twiga imekuwa si nzuri.
Hiyo
inatokana na mwenyekiti wake ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji
kupata misukosuko na serikali.
Kutokana na
hali hiyo kuna baadhi ya mambo na hasa yahusianayo na masuala ya kifedha ndani
ya klabu hiyo yalianza kuyumba.
Mwezi Machi
mwaka huu, Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa alikiri kuwawepo kwa
hali mbaya ya kiuchumi kiasi cha wachezaji kutolipwa mshahara wa mwezi mmoja.
Mkwassa alisema tangu Manji aingie matatani, hajawahi kufika
katika ofisi za klabu hiyo hivyo wamekuwa na wakati mgumu wa kupata fedha za
kuendesha klabu na hivyo walikuwa mbioni kuandaa utaratibu wa kuwataka
wanachama na wapenzi wa Yanga waweze kuichangia ili iweze kutimiza malengo yake
ya kutetea ubingwa wa ligi kuu.
Kama hiyo
haitoshi, baada ya siku chache baadae
ilitangaza kuachana na aliyekuwa Mkurugenzi wake wa benchi la ufundi, Mholanzi
Hans van der Pluijm kutokana na sababu hiyo.
Ukata huo
ulipelekea pia wachezaji kugomea mazoezi kwa siku kadhaa wakishinikizwa kulipwa
mishahara yao, kabla ya kuwekwa sawa na kuendelea na maandalizi yao ya ligi kuu
bara na michuano ya kombe la Shirikisho.
Wiki iliyopita
kumeibuka taarifa za mshambuliaji wake wa kimataifa Mzambia Obrey Chirwa kugoma
kufanya kazi ndani ya klabu hiyo hadi alipwe malimbikizo yake ya mishahara ya
miezi mitatu.
Chirwa pia
alikataa kusafiri na wenzake kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa
mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi
ya, Mouloudia Club Alger uliofanyika Jumamosi
Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers ambapo walifungwa jumla ya mabao 4-0
hivyo kuondolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-1.
Hali ya
ukata ni kitu cha kawaida hasa kwa vilabu vyetu vya bongo lakini je viongozi
huwa wanalichukuliaje na hasa kwa vilabu vikubwa ambavyo vinakuwa katika
harakati muhimu.
Mpira ni
ajira yao wachezaji kwani kuna wenye familia ambazo zinawategemea hivyo kama
wasipolipwa stahiki zao ni lazima watashindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.
Ni bora ya
chirwa ambaye ameamua kujilipua mwenywe ili kufikisha salamu kwa uongozi kuliko
hao waliokaa kimya sababu hamjui wanapanga nini vichwani mwao.
Yanga
inakabiliwa na mchakamchaka wa kuwania ubiongwa pamoja na michuano ya kombe la
Shirikisho hivyo ni kipindi ambacho wachezaji walipaswa kulipwa vizuri ili
kuwekeza nguvu katika michuano hiyo.
Lakini kwa
sasa akili zao zitakuwa zikiwaza fedha tu na matokeo yake timu itajikuta
inafanya vibaya katika michezo yake na kuanza kumtafuta mchawi wakati
wanajiroga wenyewe.
Yanga ni
timu kubwa, timu pendwa yenye mashabiki
wenye hadhi na madaraja tofauti katika
ukanda wa Afrika mashariki na Kati ambao
wakiamua wanaweza kuichangia klabua yao ili kulipa mishahara ya wachezaji na
shughuli nyingine za klabu.
Kinachoonekana
ni mawasiliano duni baina ya uongozi wa klabu na wadau wake kwani naamini kuna
matajiri wengi sana ambao wanaweza kuokoa jahazi, lakini uongozi umeamua
kumuachia mzigo huo manji pekee tu kitu ambacho sio sahihi kabisa licha ya kuwa
ni mfadhili wao.
Hivyo ni
wakati wa viongozi kuamka na kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na hali hiyo
ili kuhakikisha wachezaji wanapata stahiki zao na kazi ibaki kwao kutimiza
wajibu wao uwanjani.
Kwa kuacha
hali ibaki hivyo hivyo mwisho wa siku itawagharimu maana leo kaanza Chirwa,
kesho atakuja Tambwe (Hamis), na mwisho
wa siku timu nzima, sasa ikifikia huko unadhani timu itakuwa na mafanikio tena?
Kauli mbiu
ya Yanga ‘Daima Mbele nyuma Mwiko’
nadhani ndio ifuatwe kwa kuweka sawa kasoro ndogondogo kama hilo suala la
mishahara ili baadae wasije patwa na Matende!