Na Dina Ismail
KWA karibu takribani
miaka minne sasa, michuno ya soka ya kombe la Taifa maarufu kama ‘ Taifa Cup’ imeshindwa kufanyika.
Michuano hiyo ambayo ambayo ilianzishwa waka 1964
ikijulikana kama Sunlight Cup ilikuwa na
lengo la la kuvumbua na kukuza vipaji
vya vilivyojificha katika mikoa hiyo.
Pia michuano hiyo ililenga kuamsha na kuhamashisha michezo
na hasa mpira wa miguu katika mikoa hiyo kwa lengo la kupata wachezaji ambao
baadae wataunda kikosi cha timu ya Taifa ya Bara ambacho kitaiwakilisha nchi
katika michuano ya Chalenji.
Kupitia michuano hiyo tumepata kushuhudia kuibuka kwa
wachezaji mbalimbali ambao leo hii wameweza kuandika historia katika ramani ya
soka hapa nchini.
Kama hiyo haitoshi mivhuano hiyo imeweza kuleta hamasa kwa
hata baadhi ya mikoa ambayo imekuwa haisikiki katika medani ya soka kuamka
kutokana na kuunda timu ambayo inauwakilisha mkoa katika michuano hiyo.
Aidha michuano yab kombe la Taifa, inatumika pia kuleta
umoja, ushirikiano na upendo sambamba na burudani ambayo baadhi ya mikoa
imekuwa ikiikosa kutokamna na kukosa kushuhudia michuano mbalimbvali na hasa ya
ligi kuu bara.
Chini ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) michuano hiyo
imekuwa ikifanyika na kuna nyakati
imeshindwa kufanyika kutokana na sababu mbali mbali na hasa kukosekana kwa
wadhamini wa michuano hiyo.
Mara ya mwisho michunao hiyo ilifanyika mwaka 2011 ambapo
kampuni ya bia Tanzania (TBL) ilikuwa ikiidhamini michuano hiyo kupitia
vinywaji vyake tofauti kuanzia mwaka 2005.Mara ya mwisho ilifanyika mwaka 1994.
Hata hivyo, mpaka sasa TFF imeshindwa kabisa kufanya
jitihada zozote za kuhakikisha michuano hiyo inarejea tenja ili kurejesha hadhi
ya kabumbu hapa nchini.
Kwamba, kuna
mikoa ambayo haina timu
zinazoshiriki Ligi Kuu mfano mkoa wa
Singida ‘Kindai United’uliotwaa ubingwa huo mwaka 2010, iliweza kutoa upinzani
mkubwa na hata kutwaa kombe.
Kama hiyo haitoshi hata katika usajili wa wachezaji kulikuwa
na ushindani wa hali ya juu kama usajili wa ligi kuu bara ambako baadhi ya
wachezaji walijikuta wakigombaniwa na mikoa zaidi ya mmoja na mwisho wa siku
suala la kucheza wapi lilibaki kwa mchezaji.
Raha ilikuwa kwa timu ya mkoa wa Dar es Salaam ‘Mzizima
United’ katika usajili kusheheni nyiota
wengi wanaocheza ligi kuu bara na hasa Simba na Yanga, kabla ya baadaye
kugawanywa katika mikoa mitatu yaani Temeke, Ilala na Kinondoni.
Kupitia michuano hiyo ambayo ilikuwa na msisimko wa aina
yake, tulipata kuona ushindani wa hali ya juu toka kwa timu shiriki ambapo kila
mkoa ulijitahidi kusajili wachezaji wazuri ambao waliweza kutoa ushindani
mkubwa kwa timu pinzani.
Kwa vile michuano hiyo ilikuwa inafanyika kipindi ambacho
ligi imesimama, baadhi ya vilabu pia viliitumia kupata wachezaji ambao
iliwasajili katika vilabu vyao.
Kwa mantiki hiyo, tangu kusimama kwa michuano hiyo hamasa ya
soka imekosa msisimko zaidi imebakiki kwa mechi za Simba na yanga tu kidogo na
timu ya Taifa.
Hivyo ni vema kwa TFF
kufanya kila liwezekano kwa kuongea na makampuni makubwa ambayo yataweza kusaidia kufanyika kwa michuano hiyo kwa mara nyingine na fursa
kwa wadau wa soka mikoani kupata
burudani ya aina yake.
Hawa ndio mabingwa wa Taifa Cup Pwani ( 1964), Tanga (1965), Kilimanjaro
(1966), Pwani (1967, 1968), Tanga (1969), Morogoro (1970), Kilimanjaro (1971),
Pwani (1972),Tanga (1973), Morogoro (1974)Dar es Salaam (1975,1976,1977),
Kilimanjaro (1981,1983), Mwanza (1984,1985), Dar es Salaam (1986,1987,1998).
Mwak 1999 hadi 2004 haikufanyika kabla ya mwaka 2005 Mbeya
kuwa bingwa, 2006/2007 bingwa alikuwa Dar es Salaam, Ilala (2008, 2009),
Singida (2010) na Mbeya (2011).