Na Dina
Ismail
LICHA ya
ukongwe na umaarufu ilizonazo , vilabu
vya Simba na Yanga vinaongoza kwa kuua vipaji vya wachezaji hapa nchini.
Ndiyo! Simba
na Yanga ambazo ni mahasimu wa jadi nchini zinaongoza kwa kuua vipaji na kama
wachezaji wasiposhtuka mapema tutapoteza vipaji vingi.
Timu hizo
zenye umri wa miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, zamani zilikuwa na historia
nzuri ya kulea wachezaji wenye vipaji kwa muda mrefu tofauti na sasa.
Sijui ni
utandawazi, kukua kwa soka au ulimbukeni
ndio kunakopelekea hali hiyo kwani hali hiyo imekuwa ikishika kasi kila
uchwao.
Tanzania
imejaaliwa kuna na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lakini wengi wao
wanajikuta wakipotea baada ya kujiunga Simba au Yanga.
Ukiangali
kwa haraka haraka , kuna wale ambao walipitia katika vituo vya kukuza na
kuendeleza soka za vijana au walipandishwa toka katika timu za vijana na
kusajiliwa kuzicheza klabu hizo.
CHANZO:
Vilabu hivyo
kuwa na uwezo mkubwa wa fedha, hufanya kila jitihada za kusajili wachezaji
wazuri kwa lengo la kuimarisha vikosi vyao katika michuano mbalimbali.
Kamati za
usajili za kila klabu zitaingia msituni kusaka wachezaji wazuri ambao wanaona
watafaa kuzichezea.
Hapo sasa kuna makundi mawili, kuna walio kwa ajili ya kuzichezea tu klabu
hiyo ili kujipatia umaaarufu na pesa na kuna kundi la ambao wapo wenye malengo ya kufika mbali kupitia
vilabu hivyo.
Katika hilo;
mchezaji huyo atasota mchangani , wilayani na hata mkoa akijifua na hatimaye
kuonwa na moja ya timu za Ligi Kuu na kusajiliwa.
Ataichezea kwa nguvu zake zote timu yake hiyo iwe ya
daraja la kwanza au ligi kuu.Lakini akili yake ni kusajiliwa Simba au Yanga!
Baada ya kusajiliwa
na moja ya vigogo hao huko ataenda kukutana na changamoto nyingi ambazo bila
umakini atajikuta ndio basi tena.
Kuna ambaye
atafanikiwa kuingia kikosi cha kwanza, kuna atakayebaki kwa ajili ya mazoezi tu, sasa bila kuchekecha
akili ndio itakuwa mwisho wake.
Kundi la
Pili linaundwa na wachezaji ambao wanajielewa.Haijulikani kapitia njia ipi
mpaka kusajiliwa Simba au Yanga.
Yeye akili
yake ni kufika mbali katika medani ya soka, huyu hata akikumbana na changamoto
kwenye vilabu hivyo atakabiliano navyo na mwish wa siku atafanikiwa tu.
Hii ndio
aina ya wachezaji wanaofika mbali kwani baada ya kuingia katika utawala wa
Simba na Yanga.
Na
tumeshudia kuwepo kwa baadhi ya wachezaji ambao
hucheza kwa nguvu zote hasa pale timu yake inakapokutana na Simba au Yanga,atafanya
kila awezalo ili aweze kuvutia na kesho atafutwe.
Hapo
inaonesha lengo la wachezaji wengi ni kuzichezea Simba au Yanga na sio kuwa
mchezaji mwenye lengo la kufika mbali.
Tabu inakuja
atakaposajiliwa changamoto atakazokutana nazo Simba au Yanga ndizo
zitakazomfanya abaki kikosi cha kwanza au asugugue benchi na kujibidiisha zaidi
ili siku moja afanikiwe kusonga mbele.
Sio rahisi kupata namba katika kikosi cha kwanza kama
alivyofikiria kabla.Hiyo inatokana na kila idara kusheheni wachezaji wazuri na
wenye uwezo wa hali ya juu.
Hapo inakuwa
kama wanacheza bahati nasibu kwani kila mwenye bahati ndiye atakayekuwa chagua
la kocha na hivyo kupata namba katika
kikosi cha kwanza.
Kwa mchezaji
mwenye malengo kama hatobahatika kuingia kikosi cha kwanza, atashtuka mapema na
kujiongeza zaidi ili aweze kutimiza lengo lililompeleka hapo.
Lakini kuna
watakaobweteka kwa kuendelea kusugua benchi, mradi mwisho wa mwezi ATM inasoma
yeye hajali.Mwisho wa siku unakumbwa na fagio mwisho wa msimu.
Wachezaji
wengi wa Tanzania wanapotea baada ya kuingia Simba au Yanga kwani huko watakutana na kila aina ya tabia
ambazo zinasababishwa na umaarufu walionao, uwezo na uzoefu.Hivyo baadhi
hujisahau!
Suluhisho
Mchezaji
anatakiwa kutumia akili ya ziada ili
kuweza kufika mbali kinyume na hapo itabaki katika historia tu.