WAANDISI wa habari wanatarajiwa kujumuika pamoja kwa mara nyingine katika tamasha la aina yake linalotarajiwa kufanyika Desemba 19 katika viwanja vya Posta na simu, Kijitonyama.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa wanahabari kukutana katika tamasha linalowahusu ambapo awali walikutana katika tamasha lililofanyika desemba 5 katika ufukwe wa msasa.
Tamasha linalokuja limeandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain na litahusisha michezo mbalimbali, sambamba na burudani ya muziki.
Meneja Uhusiano wa Zain, Muganyizi Mutta, alisema hatua hiyo ni katika kutambua mchango wa vyombo vya habari kwa jamii katika kuhabarisha, kushawishi na hata kuburudisha.
"tumeona ni kitendo cha uungwana kwao kuonyesha thamani waliyonayo wanahabari kwa kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo", Alisema.
Kampuni ya Capital Plus International (CPI) ndio waratibu wa tamasha hilo.
HAYA mamaa Khadija Kalili, Happy Katabazi, Irene Mark, Asha Kigundula, Angela Msangi, Elizabeth Mayemba, na wengine kaeni mkao wa kula .
“Zain chini ya uratibu wetu imedhamiria kuwapa wanahabari burudani ya kipekee kwani mchango wenu kwetu pia umekuwa wa kipekee,” alisema Waziri.