DAVIS MOSHA
ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Soka ya Yanga Davis Mosha ameanzisha taasisi iliyolenga kusaidia watoto yatima kupitia michezo inayokwenda kwa jina la ‘Africa Soccer Aid’. Mosha amesema kupitia taasisi hiyo timu mbalimbali kutoka barani Ulaya zitakuja nchini kucheza na timu ka Simba, Yanga na nyingine za nchi jirani na fedha zitakazopatikana watapewa walengwa.
Alisema tayari ameshafanya mazungumzo na timu kadhaa nchini Uingereza huku timu kama Liverpool, Stoke City, Newcastle United, West Ham United, Tottenham Hotspurs zimeonyesha nia ya kuja nchini.