TUZO KWA WANAMICHEZO BORA WA TASWA KWA MWAKA 2011 KUTOLEWA MEI 6

KATIBU MKUU WA TASWA AMIR MHANDO KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA TUZO ZA WANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2010, KUSHOTO NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI JOSEPH KAPINGA NA KULIA NI MHAZINI SULTAN SIKILO

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Mei 6 mwaka huu kitatoa Tuzo kwa Wanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2010, sherehe zitakazofanyika ukumbi wa NSSF Waterfront, Dar es Salaam. Kamati ya Utendaji ya TASWA iliyokutana Jumamosi Machi 26, mwaka huu imeamua suala la mchakato wa kuwapata wanamichezo hao lifanywe na kamati maalum nje ya Kamati ya Utendaji ya TASWA lengo ikiwa ni kupanua wigo na kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika jambo hili nyeti. Jukumu la Kamati ya Utendaji ya TASWA itakuwa ni kuhangaika na mambo ya wadhamini na masuala mengine yahusuyo sherehe hizo ambazo tunataka ziwe za aina yake. Kutokana na msingi huo Kamati ya Utendaji ya TASWA imeteua majina 15 kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari, mawili kutoka Kamati ya Utendaji ya TASWA na moja kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kusimamia tuzo hizo mwaka huu. Ikumbukwe TASWA iliamua kubadili mfumo wake wa utoaji tuzo hizo, ambapo kila chama cha michezo kinawasilisha TASWA majina matatu ya wanamichezo wake waliofanya vizuri mwaka jana, ambao mmojawao atakuwa ndiye mshindi wa mchezo husika kwa mwaka jana. Pia kila mshindi miongoni mwa wanamichezo hao atashiriki kuwania tuzo ya Mwanamichezo wa Bora wa Mwaka 2010. Ambaye kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni mshindi wa jumla. Kwa hiyo wafuatao ndio wataunda Kamati ya TASWA ya Kusimamia Upatikanaji wa Wanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2010. Mwenyekiti wa Kamati atakuwa Masoud Sanan, ambaye ni Mhariri wa gazeti la Spotistarehe, ambaye ni mzoefu katika masuala ya taaluma ya habari, hivyo uzoefu wake utsaidia sana kufanikisha tuzo ya mwaka huu. Katibu wa kamati atakuwa Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA na Mhariri wa Michezo wa gazeti la HabariLeo, uwepo wake kama Mtendaji Mkuu wa TASWA utakuwa kiungo muhimu kati ya chama na kamati. Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Juliana Yassoda atakuwa Mshauri wa kamati ya tuzo kutokana na uzoefu wake katika masuala ya michezo na hasa vyama vya michezo.

Orodha kamili ya wanaounda kamati ni kama ifuatavyo.

1.Amour Hassan-Mhariri Nipashe

2. Rashid Zahoro-Mhariri Mzalendo

3. Alex Luambano-Clouds FM

4. Tulo Chambo-Mhariri Tanzania Daima

5. Muhidin Michuzi-Daily News

6. Chacha Maginga-TBC1

7.Frank Sanga-Mhariri Mwanaspoti

8.Saleh Ally-Mhariri Kiongozi Championi

9. James Range-Star TV

10.Editha Mayemba-Radio Tumaini

11. Said Kilumanga-Chanel Ten/Magic Radio

12.Rehule Nyaulawa-Mkurugenzi Times FM

13. Angel Akilimali-Meneja Vipindi Radio Uhuru

14. Masoud Sanan-Mhariri Spotistarehe

15. Amir Mhando-Katibu Mkuu TASWA

16. Alfred Lucas-Mjumbe TASWA

17.Patrick Nyembela-EATV

18: Juliana Yassoda-Naibu Mkurugenzi Idara ya Michezo

Ahsante

Amir Mhando

Katibu Mkuu TASWA

28/03/2011

Post a Comment

Previous Post Next Post