DULLY SYKES ACHARUKA 'BONGO FLEVA' KUWA MIITO YA SIMU


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Abdulwahid Sykes maarufu kama ‘Dully Sykes’ au ‘Brotheman’(Pichani kushoto) ameishutumu kampuni moja ya simu kutumia wimbo wake unaotamba sasa ‘Bongo Fleva’ kama miito ya simu ‘caller tunes’ za wateja wake.

Msanii huyo alisema anashangazwa na kampuni hiyo kutumia wimbo wake bila makubaliano kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

"Nashanga jamaa (jina kapuni) wameuchukua wimbo wangu bila ridhaa yangu na kuuweka kwenye caller tunes zao, wakati wao wataingiza mkwanja mi sipati kitu”.

“Mimi nimejisajili pamoja na track (wimbo) wangu kwa vyombo vinavyohusika kama ni mmiliki halali wa wimbo wa Bongo Flava na yoyote atakayeutumia bila ridhaa yangu anavunja sheria", Alisema Dully.

Post a Comment

Previous Post Next Post