TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 7, 2011
MAPATO SIMBA v JKT RUVU
Mechi namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na JKT Ruvu iliyochezwa Aprili 6 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeingiza sh. 21,106,000. Mapato hayo ni kutokana na watazamaji 4,264 waliolipa kutazama mechi hiyo. Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 15,000 kwa VIP, sh. 8,000 Jukwaa Kubwa, sh. 5,000 Jukwaa la Kijani n ash. 3,000 Mzunguko. Baada ya kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 3,219,559 fedha iliyobaki kwa mgawanyo kwa pande zote husika ni sh. 17,886,441. Jumla ya gharama za awali za mchezo ni sh. 2,275,000 wakati kila timu ilipata sh. 4,683,252. Uwanja sh. 1,561,084, TFF sh. 1,561,084, gharama za mchezo sh. 1,561,084, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 156,108, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 624,433 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 780,542.
Boniface Wambura
Ofisa Habari