MISS MOROGORO KUSAKWA JULAI 1

Kwa niaba ya FG ARTS PROMOTION AND ENTERTAINMENT naomba nitume kwako
taarifa ya mchakato mzima wa kumtafuta muwakilishi wa mkoa wa Morogoro
kwenye sekta ya "ulimbwende" mwaka 2011.
Tarehe 01 / 07 / 2011, katika hoteli ya Morogoro Hotel, warembo 15
watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Morogoro 2011. Shindano
litaanza saa mbili usiku hadi saa sita likishindikizwa na burudani
kabambe toka kwa timu nzima ya Tip Top Connection, pamoja na vibwagizo
babukubwa toka kwa msanii Wanne Star.
Kiingilio kitakua 10,000 Tsh kwa mtu mmoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post