MISS SINZA KUPATIKANA LEO, MAPACHA WATATU KUPAMBA ONYESHO




"MWAKA huu tunataka kuweka historia katika medani ya urembo, hata kama si kutwaa taji la Taifa basi hata kuingiza warembo wengi katika fainali za Miss TAnzania,"Hiyo hi kauli ya Titina Makutika ambaye ni mratibu wa shindano la kumsaka mrembo wa Sinza mwaka huu.
Shindano hilo limepangwa kufanyika leo katika hoteli ya Vatican iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam ambapo warembo 15 leo wanatarajiwa kupanda jukwaani kuiwania taji hilo linaloshikiliwa na Amisuu Malick.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Titina alisema ana jeuri ya kutoa kauli hiyo kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kuhakikisha wanatafuta warembo bora ambao wanaweza kufanya vema katika shindano hilo kama si kufika mbaliu.
Alisema, washiriki wa kitongoji hicho ni wamekamilika kila idara hali ambayo itawapa wakati mgumu majaji wa shindano hilo kuamua nani anastahili kuvikwa taji la Miss Sinza.
Kama hiyo haitoshi, warembo hao wamekuwa kambini kwa kipindi kirefu wakijinoa kwa ajili ya shindano hilo ambalo kwa wale watakaohudhuria siku ya leo litakuwa na usimulizi wa aina yake.
"Unajua urembo si sura wala kujua kutembea jukwaani, hii fani ina mambo mengi ndiyo maana poamoja mafunzo ya kawaida ya masualka ya urembo tumekuwa tukiwapa mafunzo ya iana mbalimbali washiriki ili kuhakikisha wanakuwa mabalozi bora mara baada ya mashindano,"Alisema.
Mratibu huyo anaongeza kuwa kwa kiasi kikubwa maandalizi ya shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Calapy Entertainment yamekamilika huku kila mrembo akitamba kuibuka mshindi.
:"Kila kitu kipo vizuri na hata warembo wamepikwa na kuiva hasa chini ya ukufunzi wa Amisuu akiisaidiana na Beatrice Joseph ambaye alikuwa Miss Ruvuma 2006 na Miss Tanzania kumi bora kwa mwaka huo.

Washiriki wanaotarajiwa kupanda jukwaani hii leo ni pamoja na , Stella Moris (20), Husna Maulid (29), Hanifa Halfani (18), Naomi Jones (19), Joyce Raphael (18), Anna Gerald (20) Mariam Almas (20) na Felista Philip (19).
Wengine ni Pamela Gordian (19), Winnie Gerlad (18), Grace Revocatus (20), Hellen Masawe (18), Stella Premsingh (20) , Jacquelin Joachim (19) na EveLyna Rwandala (20)
Alisema mshindi atapata zawadi ya shiling 600,000 wa pili anajinyakulia kitita cha shilingi 400,000, ambapo watatu atashinda shilingi 300,000 na wa nne na watano kwa pamoja watapata shilingi 200,000, huku washiriki waliosalia kila mmoja ataondoka na kifuta jasho cha shilkingi 100,000.
Shindano hiloambalo limedhaminiwa na Vodacom, Redds,Fabeck, Jambo Leo, Clouds Fm na Full Shagwe blogspot.com, litapambwa na burudani ya muziki toka kundi la Mapacha Watatu.
Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post