WAKATI Yanga ikitangaza kuwa msshambuliaji Oscar Joshua ni mali yake halali, Ruvu Shooting imekuja juu na kiudai kuwa Joshua ni halali yao na wamewasilisha jina lake kwenye usajili waliowasilisha Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).
Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisema kwamba licha ya Yanga kumtumia mchezaji huyo kwenye michuano ya Kagame lakini haikuwa halali yao.
Alisema kweli Yanga waliwasailiana na uongozi wakiwa na nia ya kutaka kumsajili badala yake walishindwa kufuata taratibu zinazostahili.
"Dada Joshua ni mchezaji wetu halali na jina lake tunaliwasilisha TFF muda si mrefu kama mmoja ya wachezaji wetu,"Alisema Bwire.
Kufuatia msigano huo, TFF imeazimia kuliwasilisha suala hilo kwa kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji ili liweze kushughulikiwa.