UONGOZI wa klabu ya Villa Squad leo unatarajia kusikiliza utetezi wa wachezaji wake watano waliowasimamisha kutokana na utovu wa nidhamu, mkutano utakaofanyika kwenye hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Villa, Jumanne Matipa alisema juzi Villa iliwasimamisha wachezaji hao kutokana na utovu wa nidhamu katika baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara inayoendelea hapa nchini.
Matipa aliwataja wachezaji hao ni pamoja na Shai Mpala, Mohamed Lupatu, Zubery Daby, Benard Mganga na Abbas Nassor.
Aidha Matipa alisema uongozi wa Villa una wasiwasi na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuhusishwa katika njama zilizowakuta wachezaji hao ambako pia alisema watawachukulia hatua viongozi watakaobainika.