MJUMBE
wa kamati ya utendani ya klabu ya soka ya Yanga, Mohammed Bhinda (Pichani) amekana
kuhusika na ubadhirifu wa fedha za mapato ya mechi ya Ligi ya mabingwa Afrika
baina ya Yanga na Zamalek uliofanyika jumamosi iliyopita katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam.
Aidha,
Bhinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya klabu ya Yanga amekana
kuwa hajasimamishwa uongozi ndani ya klabu hiyo kama baadhi ya vyombo vya habari
vilivyoripoti hivi karibuni.
Bhinda alisema anashangazwa
na taarifa hizo zisizo na ukweli wowote ambazo anaamini zinalengo la kumchafua
yeye, klabu ya Yanga pamoja na Wanayanga kwa ujumla.
Alisema
kuwa, siku chache kabla ya timu hizo kuvaana mkurugenzi wa Primetime Promotion
ambao walikuwa wanaratibu mechi hiyo, Joseph Kusaga ambaye alimuomba amsaidie
kuuza tikeki za mchezo huo katika maeneo ambayo ni sumbufu ambapo alikubali na
kuingia mkataba kama Bhinda na si mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.
“Sikuona
haja ya kumkatalia kwa sababu uongozi ulinipa jukumu la kushirikiana nao kwa
namna moja ama nyingine, hivyo nilitafuta baadhi ya wanachama waaminuifu wa
Yanga na kuwapa kazi hiyo ambayo waliifanya kwa uadilifu mkubwa na mwisho wa
siku zilipatikana shilingi mil.71,544,000,”Alisema.
Bhinda
aliongeza kuwa baada ya makabidhiano ya pesa hizo na tiketi zilizobaki aliomba
kurudishiwa fedha zake ambazo alitumia katika kuwalipa posho maofisa wa polisi,
wakata tiketi na usafiri ambapo alirejeshewa, huku Kusaga akimpongeza kwa kazi
nzuri aliyoifanya na hasa ikizingatiwa kuwa vituo alivyopewa huwa vina
usumbufyu mkubwa.
“Sina
matizo na Primetime Promtions, hata wanayanga niliowapa kazi hiyo l;akini nashangaa
taarifa hizo zinatoka wapi,napenda kuwaondoa wasiwasi wanayanga wenzangu kuwa
mimi bado mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga, sijasimamishwa na nitaendelea kuwa mwanachma wa
Yanga,”alisema Bhinda.