Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo
ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji
(Mambas) itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni
sh. 3,000.
Jumla viti 36,693 (rangi ya
bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa kiingilio hicho katika uwanja huo
wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wameketi.
Viingilio vingine ni sh.
5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 15,000 kwa VIP B
wakati kwa watakaokuwa miongoni mwa watakaokaa katika viti VIP A ambavyo viko
748 tu watalazimika kulipa sh. 20,000 kwa kila mmoja.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku
moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo
cha mafuta cha Bigbon kilichopo Msimbazi (Kariakoo), mgahawa wa Steers ulioko
Barabara ya Samora/Ohio, Kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo na Uwanja wa
Taifa.