Mkoa unaotaka kuwa mwenyeji wa fainali za
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoshirikisha timu tisa bora za ligi hiyo
unatakiwa kutoa sh. milioni 25 ambazo ni gharama za kuendesha fainali
hizo.
Haki ya kuwa mwenyeji wa
fainali hizo iko wazi kwa mikoa yote wanachama wa TFF ingawa tayari ipo minne
ambayo imeshatuma rasmi maombi ya kuandaa fainali hizo. Mikoa hiyo ni Mbeya,
Mwanza, Ruvuma na Tabora.
Kwa mikoa ambayo itakuwa
tayari kuwa mwenyeji kwa maana ya kutimiza sharti hilo la kutoa kiasi hicho cha
fedha inatakiwa iwe imefanya hivyo kufikia Machi 15 mwaka huu.
Pia kumefanyika mabadiliko ya
kuanza fainali hizo, sasa zitaanza Machi 31 mwaka huu badala ya Machi 17 ambayo ilitangazwa awali.
Boniface Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)