Kocha mkuu wa Yanga ,Mserbia Kostadic Papic juzi
alitoa zoezi la wachezaji wake kupiga pelnati kwa wingi kutokana na kuhofia
uenda timu hiyo ikatoka sare ya bao 1-1
na mshindi akaamuliwa kwa matuta .
Akizungumza
jijini jana , kocha huyo alisema kuwa mara nyingi kikosi hicho kimekuwa
kikipata shida sana
pindi inapofika wakati wa kupiga pelnati.
Kocha huyo alisema kuwa zoezi hilo lilifanywa na wachezaji wote ambapo
wengi wao walikuwa wanashindwa kufanya vile inavyotakiwa .
“Mara nyingi inapofika wakati wa matuta wachezaji
wengi ushindwa kufanikisha baoa jambo ambalo linatia shaka”alisema Papic
Kocha huyo alisema kuwa anaisi katika mchezo huo dhidi
ya Zamalek timu hiyo zitaweza kutoka sare ya bao 1-1 ndiyo maana ameamua
kuendesha zoezi hilo
.
Katika mazoezi ya juzi na jana asubuhi wachezaji waliokuwa wakionyesha uwezo wa
kufunga wakati wa upigaji walikuwa ni Nadir Aroub ‘Cannavaro’,Hamis Kiiza,
Keneth Asamoah na Devis Mwape.
Katika hatua nyingine msemaji wa klabu hiyo Luis Sendu
alisema kuwa upande wa mchezaji Haruna Niyonzima anatarajiwa kutua jijini kesho
mapema iliaondoke na kikosi jioni .
Sendeu alisema kuwa lazima mchezaji huyo awasili hapa
jijini kwanza ndipo aondoke hata kama
akichelewa na kukuta kikosi hicho kimeondoka.
“Rwanda
hakuna ndege ya moja kwa moja kwenda Misri hivyo lazima Haruna aje hapa nchi
hivyo hata kama kikosi kitakuwa kimeondoka
basi atapanda ndege ya moja kwa moja kuja Misri”alisema Sendeu