OFISA habari wa Yanga, louis Sendeu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mechi yao ya kesho dhidi ya Villa Squad kuhamishiwa Uwanja wa Taifa
WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga kesho wanakwaana na Villa Squad katika mchezo wa ligi hiyo, Shirikisho la soka
Tanzania (TFF) limehamisha mchezo huo kutoka dimba la Chamazi hadi Uwanja wa
Taifa, imefahamika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kuwa mabadiliko hayo
yanafuatia wamiliki wa Uwanja wa Chamazi,Azam Fc kuandika barua TFF kuomba
mechi hiyo isipigwe katika dimba hilo
kwa hofu ya kutokea vurugu.
“Ndiyo hivyo Villa kama wenyeji
wetu huwa wanatumia uwanja wa Chamazi lakini mmiliki wake (Azam FC) ameandika
barua TFF kuomba mechi yetru isipigwe huko kwa madai kuwa wanahofia kutokea
vurugu kutoka kwa mashabiki wetu,”Alisema Sendeu.
Azam Fc wamelazimika kugomea uwanja wao wakihofia Yanga
kuendeleza vuruga walizozifanya mmwishoni mwa wiki iliyopita walipokwaana
katika dimba la Taifa na Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.