KOCHA
Msaidizi wa timu ya Moro United ‘Watoto wa Tabata’ Yusuph Macho ‘Muso’, amesema
vurugu zilizofanywa na wachezaji wa klabu kongwe ya Yanga katika mchezo wao dhidi
ya Azam Fc zinapaswa kulaaniwa na kila mpenda michezo nchini.
Macho,
nyota wa zamani wa Simba na Yanga, aliyasema hayo jijini Dar
es Salaam jana, wakati akizungumza na Tanzania Daima kwa
njia ya simu, kuhusiana na vurugu zilizoanza kujitokeza katika ligi kuu ya soka
Tanzania
bara.
Alisema,
kinachomsikitisha ni kuona, vurugu hizo zinafanywa na wachezaji wa timu
zinazoitwa kongwe hapa nchini, jambo linalotoa picha mbaya kwa timu nyingine na
kwa vijana wanaochipukia katika ulimwengu wa soka.
“Ni muhimu
hasa kwa hawa wachezaji wa timu kubwa na wenye majina makubwa, kuzuia mihemko yao kwa kuwa jamii inawaangalia wao kama
mifano ya mambo mazuri, sasa wanapofanya vitu visivyoeleweka ni kudhalilisha
fani ya soka nchini,” alisema Muso.
Aliongeza
kuwa, wachezaji waliodhibiwa wasipoteze muda wao kumtafuta mchawi, bali wakae
na kutuliza akili kwa ajili ya kuhakikisha hawarudii makosa kama
hayo, kila watakapopata fursa ya kuingia uwanjani.