MSANII wa Filamu nchini, Kajala Masanja (pichani)na mumewe Faraja
Chamba jana walijikuta wakiifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakikabili na makosa matatu likiwemo kosa la kutakatisha fedha haramu.
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKUKURU),
Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alidai kuwa washtakiwa hao ambao
ni wanandoa na wanatetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa wanakabiliwa
na makosa matatu.
Wakili Swai alidai
kuwa kosa la kwanza ni la kula njama
kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya
mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote kwa pamoja
walitenda kosa hilo la kula njama la kuamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es
Salaam.
Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha
isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo
kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa ya mwaka 2007.
Alidai shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo
walilitenda siku hiyo ya Aprili 14 mwaka
2010 huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Hata hivyo mshtakiwa wa pili (Chambo) wakati wanasomewa
mashtajka hayo jana hakuwepo mahakamani
kwasababu yupo gerezani kwakuwa
anakabiliwa kesi nyingine ya utakatishaji fedha ambayo ipo katika mahakama hiyo
na kwa mujibu wa sheria kosa la kutakatisha fedha halina dhamana.
Kajula alikanusha mashtaka hayo na wakili Swai alidai
upelelezi bado haujakamilika.Hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo Aprili 20 mwaka
huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa na akaamuru Kajala arudishwe rumande kwa
sababu kosa la kutakatisha fedha linamkabili halina dhamana kwa mujibu wa
sheria.