Mcameruni, Kengne Alain Thierry
WACHEZAJI watatu kutoka nchi za Cameroon
na Gabon wapo nchini kwa
ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa soka la Tanzania kabla ya kuangalia timu
watakayoweza kuichezea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakala wa wachezaji
hao Mussa Abdallah alisema wachezaji hao wapo nchini kwa siku kadhaa ambapo
pamoja na mwenendo huo wanaangali hali ya hewa ya Tanzania .
Alisema nyota hao wanacheza katika klabu ya Missile Fc
ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya huko iliyomalizika hivi karibuni na timu
hiyo kushika nafasi ya tatu.
Aliwataja wachezaji hao ni pamoja na washambuliaji Kengene Thiery na Nkamseu Herve
Jean kutoka Cameroon na beki
Moussono Charly kutoka Gabon
ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon .
mbona kwenye habari ya sendeu anaandika habari huyo sio mchezaji huyo mwandishi wako
ReplyDelete