SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesema adhabu walizopewa
wachezaji wa klabu ya soka ya Yanga ni sahihi kwani kumpiga mwamuzi ni utovu wa
nidhamu.
Hatua hiyo inafuatia Yanga kulalamikia adhabu ya vifungo na
faini waliyopewa wachezaji wake watano kutokana na kumpiga mwamuzi Israel
Nkongo mmwishoni mwa wiki iliyopita wakati Yanga ilipocheza na Azam Fc katika
mechi ya Ligi Kuu Bara kwewnye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa TFF Leodger
Tenga alisema wachezaji hao waliadhibiwa kwa mujibu wa sheria na Kanuni za soka
na mchezaji yoyote atakayeonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu ataadhibiwa kwa
mujibu wa kanuni.
“Wachezaji kumpiga mwamuzi si tu kinyume cha sheria ni utovu
wa nidhamu…haya mambo yalikuwa zamani lakini kwa sasa mambo hayo yanatakiwa
kufanywa katika mechi za mchangani lakini si kwa wachezaji ambao tunateghemea
siku moja wakacheze soka la kulipwa nje ya nchi,”Alisema Tenga.