VINARA wa ligi kuu soka Tanzania BAra, Simba wameingia kambini kujindaa na mechi yao dhidi ya Toto Africa ya Mwanza utakaopigwa jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaka amesema kwamba kikosi chao kipo Bamba Beach kikijiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kama ilivyo michezo mingine ya ligi hiyo.
Amesema kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyosalia na hivyo kunyakua ubingwa wa msimu huu.
Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 40, huku nafasi ya pili inashikiliwa na Azamu Fc yenye pointi 38 na Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35.
HIVI MWANANGU HUWA MNAWAOGOPA SANA HAWA WATOTO WA MWANZA EEEH?
ReplyDeleteKWELI LAKINI MAANA HUWA WANAWATESA SANA KWA MIGOLI MINGI MINGI
MDAU WA BOMBA LA UHURU,REVERE,MASACHUSSETTS,USA