MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga wametamba kuionyesha ukongwe wao wa Ligi hiyo Azam Fc ambayo kesho watakutana kwenye mchezo wa ligi hiyo utakaopigwa katika dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kuwa kikosi chao kipo vizuri kwa
mchezo huo ingawa utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na ubora walionao Azam
lakini na ushindi kwao muhimu.
“Kila mtu nafahamu ubora wa
Azam lakini hilo halitutii hofu ya kuona tumeshafungwa kwani ng’ombe hazeeki
maini, tunaiheshimu sana Azam lakini dakika 90 ndizo zitaamua nani
zaidi,”Alisema Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa
wachezaji wa timu hiyo wapo katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huo
isipokuwa Salum Telela na kipa Yaw Berko waliokuwa majeruhi kwa sasa hali zao
zimetengemaa na wameanza mazoezi mepesi.
HIVI MWANANGU HUWA MNAWAOGOPA SANA HAWA WATOTO WA MWANZA EEEEH?
ReplyDeleteKWELI LAKINI MAANA WANAWATIAGA ADABU KWA MIGOLI MINGI MINGI.
MDAU WA BOMBA LA UHURU,REVERE,MASACHUSETTS,USA