MAHASIMU wa jadi nchini timu za Simba na Yanga leo zitaendeleza harakati za
kuwaniubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo watashuka katika viwanja
viwilitofauti nchini.
Wakati Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 41 itashuka katika dimba la Jamhuri mjini Dodoma kukwaana na maafande wa
PolisiDodoma, mabingwa watetezi Yanga
wataikaribishaAfrican Lyon katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga yenye pointi 37 itacheza mechi ya leo bila nyotawake
kadhaa tegemeo ambao wamefungiwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
kwanyakati tofauti kutokana na vurugu katika mchezo wao na Azam Fc mwishoni
mwawiki, huku pia ikiwa na machungu ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo huo.
Kwa mantiki hiyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa naushindani
mkubwa kwani Yanga itahitaji kupoza machungu ya kupoteza mchezouliopita na
hatimaye kujipatia pointi tatu muhimu ambazo zitawaweka kwenyemazingira mazuri
katika kuelekea kutetea ubingwa wao.Lakini Yanga hataikishindinda itaendelea
kubaki nafasi ya tatu kwani Azam Fc
inayoshika nafasi ya pili ina pointi 41.
Hata hivyo, Lyon nayo hawatakubali kirahisi kufungwa naYanga
kwani nayo inazihitaji pointi tatu ili kujipandisha katika msimamo waligi hiyo ambapo
kwa sasa inashikilia nafasi ya 10 ikiwa na pointi 18.
Kwa upande wa Simba, watashuka wakiwa na ari na kasizaidi ya
kutaka kurekebisha matokeo yao ya sare ya bila kufungana na Toto African mwishoni mwa
wiki hivyo kuwafanya kuwa na kibarua kigumu cha kuhakikishawanapata pointi tatu
za ugenini ili waendelee kukalia kiti sambamba nakuchochea ndoto zao za kutwaa
ubingwa.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF)limetaja viingilio vya mechi ya Yanga na Lyon itakayoanza kurindima saa
10.30jioni ambapo watakaokaa viti vya bluu na kijani watalipa 3,000, watakaokaa viti vya randi ya
chungwawatalipa shilingi 5,000, huku
watakaokaaVIP C na B watalipa shilingi sh. 10,000na VIP A watalipa shilingi
15,000.