Yanga na Simba ni miongoni mwa timu nne zitakazokuwa viwanjani
kesho (Machi 31 mwaka huu) kusaka pointi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo iko katika
raundi ya 22.
Uwanja wa Mkwakwani, jijini
Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi namba 148 kati ya Coastal Union na Yanga. Mechi
hiyo itachezeshwa na mwamuzi Rashid Msangi wa Dodoma ambaye atasaidiwa na Rashid
Lwena (Ruvuma) na Issa Malimali (Ruvuma).
Mwamuzi Amon Paul wa Musoma
ndiye atakayechezesha mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viingilio kwenye mechi ya
African Lyon na Simba ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani na bluu, sh. 5,000 viti
vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh.
15,000.
Aprili Mosi mwaka huu
kutakuwa na mechi ya VPL kati ya Azam na Ruvu JKT itakayochezwa Uwanja wa
Chamazi, Dar es Salaam. Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 1,000 kwa
mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu.