Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Machi 14
mwaka huu) limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga
kwenye mechi dhidi ya Azam.
Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye
mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo
ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.
Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na
uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya
ukarabati haraka.
TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na
washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa
vifaa hasa kutokana na ukweli kuwa mpira
wa miguu ni mchezo wa burudani.
Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo
si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita
kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.
Rungu hilo limetua Yanga Nani wa kulaumiwa?
ReplyDelete