Timu za Moro United na Villa Squad ambazo
ziko kwenye vita ya kukwepa kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
zinapambana kesho (Machi 28 mwaka huu) kwenye moja kati ya mechi mbili za siku
hiyo.
Mechi hiyo namba 153
itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Moro
United iko nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 wakati Villa Squad iko nafasi ya 14
kwa pointi zake 14.
Viingilio katika mechi hiyo
ni sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu. Mwamuzi atakuwa Andrew
Shamba akisaidiwa na Samson Kobe na Idd Mikongoti wote wa Dar es
Salaam.
Kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Arthur Mambeta wa Dar es Salaam wakati mtathmini wa waamuzi (referees
assessor) ni Emmanuel Chaula kutoka mkoani Rukwa.
Mechi nyingine ya Machi 28
mwaka huu itakayochezeshwa na mwamuzi Judith Gamba wa Arusha itakuwa kati ya
Ruvu Shooting itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko
Mlandizi mkoani Pwani.
Gamba katika mechi hiyo namba
150 atasaidiwa na Saada Tibabimale kutoka Mwanza na Hellen Mduma wa Dar es
Salaam. Mwamuzi wa akiba ni Juma Safisha wa Pwani wakati Kamishna ni Hamis
Kissiwa wa Dar es Salaam.
Mechi za Machi 31 mwaka huu
ni Coastal Union dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi ya African Lyon na
Simba.
RHINO, POLISI DAR KUANZA
FAINALI FDL
Timu za Rhino Rangers ya
Tabora na Polisi Dar es Salaam zitapambana Machi 31 mwaka huu katika moja ya
mechi za ufunguzi wa fainali za Ligi Daraja la Kwanza zitakazochezwa Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Kila siku zitachezwa mechi
mbili, moja ikianza saa 8 mchana wakati ya pili ni saa 10 jioni ambapo fainali
hiyo itamalizika Aprili 22 mwaka huu kwa timu tatu za kwanza kupanda Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) msimu ujao- 2012/2013.
Morogoro imepewa uenyeji
baada ya kulipa sh. milioni 20.5 kati ya sh. milioni 25 zilizotakiwa. Sh.
milioni 4.5 zilizobakia imekubaliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kuwa itazilipa moja kwa moja kwenye huduma zitakazotumiwa na wasimamizi wa
fainali hizo.
Mkoa mwingine ulioomba
uenyeji ulikuwa Mbeya. Lakini wenyewe hadi Machi 26 mwaka huu ambayo ilikuwa
siku ya mwisho kufanya malipo ulikuwa umeingiza kwenye akaunti ya TFF sh.
milioni 15.
Upangaji ratiba (draw)
ulifanyika jana (Machi 26 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na viongozi wa timu saba kati ya tisa
zinazocheza fainali hizo.
Mechi ya pili siku ya
ufunguzi itakuwa kati ya Trans Camp na Mbeya City Council. Aprili Mosi ni
Tanzania Prisons na Polisi Morogoro zitakazocheza mchana wakati jioni ni Mgambo
Shooting na Mlale JKT.
Aprili 2 mwaka huu ni Polisi Tabora vs
Rhino Rangers (mchana) na Polisi Dar es Salaam vs Trans Camp (jioni). Aprili 3
mwaka huu ni Mbeya City Council vs Tanzania Prisons (mchana) na Polisi Morogoro
vs Mgambo Shooting (jioni).
Aprili 5 mwaka huu ni Polisi
Tabora vs Mlale JKT (mchana) wakati jioni ni Rhino Rangers vs Trans Camp. Aprili
6 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mbeya City Council (mchana) wakati jioni ni
Tanzania Prisons vs Mgambo Shooting.
April 8 mwaka huu ni Mlale
JKT vs Polisi Morogoro (mchana) wakati jioni itakuwa Polisi Tabora vs Polisi Dar
es Salaam. Aprili 9 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Rhino Rangers (mchana)
wakati jioni ni Trans Camp vs Tanzania Prisons.
Aprili 11 mwaka huu ni Mbeya
City Council vs Polisi Tabora (mchana) na Mlale JKT vs Rhino Rangers (jioni).
Aprili 12 mwaka huu Polisi Dar es Salaam vs Mgambo Shooting (mchana) na Polisi
Morogoro vs Trans Camp (jioni).