Fabian Joseph akihojiwa na mtangazaji wa radioFive muda mfupi baada ya kumaliza
mbio za kilometa 21 za Ngorongoro Marathon zilizotimua vumbi mjini Karatu
mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa nne wa mbio za Ngorongoro Marathon,Failuna Abdi akisaidiwa kutembea
baada ya kushindiwa kutembea.
Mwanariadha maarufu nchini,Restuta Joseph akihojiwa muda mfupi baada ya kumaliza
mbio za Ngorongoro Marathon ziizofanyika mwishoni mwa wiki mjini Karatu mkoani
Arusha
.mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 za Ngorongoro Marathon,Jacklin
Sakilu akimaliza mbio zake i kwenye uwanja wa mazingira bora mjini Karatu
mwishoni mwa wiki.
Washiriki wa mbio za kilometa 21 za Ngorongoro Marathon wakijiandaa kutimua vumbi kwenye lango kuu la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mwishoni mwa wiki.
wanariadha wakitimua vumbi kwenye mbio za Ngorongoro Marathon mwishoni mwa wiki mjini Karatu (picha zote na Charles Ndagula)
Na Charles
Ndagulla,Karatu.
WANARIADHA wa
maarufu nchini wanaojiandaa kufuzu kwa mashindano ya
Olimpiki mapema julai mwaka huu,jana waling’ara vilivivyo katika mbio za
Ngorongoro Marathon baada ya kushika nafasi za juu katika
mashindano hayo ya kilomita 21.
Mashindano hayo
yanayondaliwa na Kampuni ya wakala wa Utalii ya Zara ya mjini Moshina
kudhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjani ya Tigo,yalishirikisha wanariadha
wapatao 107 na yalianzia kwenye lango kuu la kuingia watalii la Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizikia kwenye uwanja wa mazingira bora katika mji
wa karatu.
Kwa upande wa
wanaumme,Fabian Joseph alishika nafasi ya kwanza akitumia muda wa
1:03:47 huku nafasi ya pili ikikamatwa na Martin Sulle aliyetumia muda wa
1:04:26 wakati Stephano Huche mshindi w tatu wa Kilimanjaro Marathon mwaka jana
akishika nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa 1:04:30.
Mwanariadha Damian Chopa
alishika nafasi ya nne kwa kutumia muda wa 1:05:05 wakati mwanariadha Pascal
Momba alikamata nafasi ya tano baada ya kutumia muda wa saa 1:05:49.
Kwa upande wa
wanawake,Jaklin Sakilu kutoka JWTZ Arusha alishinda mbio hizo baada ya kutumia
muda wa 1:16:01 huku nafasi ya pili ikikamatwa na mwanariadha mkongwe
nchini,Restuta Joseph aliyetumia muda wa 1:18:28.
Restuta kama ilivyo kwa
Fabian pia anatumia mashindano hayo kujiandaa kufuzu kwa mshindano
ya Olimpiki wakati mwanariadha Samson Ramadhan na Zakia Mrisho wakiwa tayari
wameshafuzu.
Nafasi ya tatu kwa upande wa
wanawake ilikamatwa na Siata Romanus pia kutoka JWTZ Arusha
aliyetumia muda wa s aa 1:20:30 wakati Failuna Abdi msichana mdogo
mwenye umri wa miaka 19 akikamata nafasi ya nne kwa kutumia saa 1:21:01 na
Natali Elisante akikamata nafasi ya tano kwa kutumia muda wa saa
1:21:30.
Mbio hizo za Ngorongoro
Marathon ambazo kwa sasa zimedumu kwa mwaka wa tano,zimekuwa mahususi kwa ajili
ya kutoa ujumbe kwa jamii juu ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
Mshindi wa kwanza kwa upande
wa wanaume alipata zawadi ya pesa taslimu sh,500,000 huku wa pili akizawadiwa
sh,300,000 na mshindi wa tatu akipewa sh,150,000 huku kwa upande wa wanawke
mshindi wa kwanza akilamba 300,000,wa pili 150,000 na wa tatu
akipata sh,100,000.
Akizungumza mara baada ya
mbio hizo,kocha wa Taifa wa Riadha,Zacharia Gwandu alisema kuwa mwanariadha
Dixon Marwa ambaye hakushiriki mashindano hayo,anajindaa na marathon ya kufuzu
Olimpiki April 29 mwaka huu huko Harmburg nchini Ujeruman.
Kwa upande wake Fabian,kocha
huyo alisema kuwa,anatazamiwa kushiriki marathon ya kufuzu kwa Olimpiki Mei 13
mwaka huu katika mji Mkuu wa Jamhuri ya watu wa Zcheck wa
Prague.
Alisema kwa ujumla hali ya
kambi iliyopo Kibaha mkoani Pwani ni nzuri na kwamba wanariadha wote wamekuwa
wakihudumiwa vizuri na kwamba kambi hiyo imeanza wakati mwafaka.