Van Persie |
INGAWA Sergio Aguero alikuwa
anaumwa kifundo cha mguu, lakini inaaminika atakuwa fiti kumbeba kocha wake Roberto
Mancini leo dhidi ya Arsenal.
Joleon Lescott amepona maumivu
ya nyonga lakini inaweza kuwa ajabu kumuona kwenye kikosi cha Manchester City katika
mchezo huo muhimu.
Micah Richards anaumwa kichwa
alilazimika kuiacha mechi kati ya sare ya 3-3 kati ya City na Sunderland ikiendelea
mwishoni mwa wiki iliyopita na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Pablo
Zabaleta katika beki ya kulia.
Samir Nasri ambaye naye yuko
fiti anawania nafasi kwenye kikosi cha kwanza kucheza dhidi ya timu yake ya
zamani, baada ya kukosa mechi iliyopita.
Arsenal ina kikosi kamili na ni
kocha tu yeye mwenyewe kuchagua amtumie nani katika vita la leo.
Jack Wilshere anayeumwa kifundo
cha mguu ataendelea kuwa nje ya Uwanja, kama ilivyo kwa viungo wenzake,
Emmanuel Frimpong (goti), Abou Diaby (nyama) na Francis Coquelin (nyama). Beki Per
Mertesacker anayeumwa kifundo cha mguu pia hatacheza kwenye Uwanja wa Emirates
Leo..
JE WAJUA?
•Arsenal ilishinda mechi sita
mfululizo kabla ya kusimamishwa na QPR kwa kichapo cha 2-1 mwishoni mwa wiki
iliyopita, na miongoni mwa mechi ilizoshinda ni dhidi ya Tottenham, Liverpool na
AC Milan.
•Manchester City imekuwa butu ugenini
kwa miezi kadhaa sasa.
•Mechi zote baina ya timu hizo
zinazowania kucheza Ligi ya Mabingwa msimu huu ziliisha kwa Mancini kushinda
1-0.
•City wamefungwa mechi zote nne
msimu huu ambazo Mario Balotelli na Edin Dzeko wamecheza pamoja kikosini.
•Pamoja na kwamba City iliifunga
The Gunners katika Kombe la Ligi Uwanja wa Emirates, Novemba, mara ya mwisho
timu hiyo kuifunga Arsenal katika Ligi Kuu ilikuwa Oktoba. 4, 1975.
•Balotelli amefunga mabao kila baada ya dakika
94 msimu huu, ambayo ni kiwango kizuri katika Ligi Kuu kwa wachezaji wote ambao
wamecheza kiasi cha dakika 1000.
•Theo Walcott anafagiliwa na
mashabiki wa Arsenal, lakini winga huyo amefunga au kutoa pasi za mabao 15 katika
mashindano makubwa tangu msimu wa 2011-12 uanze. Wayne Rooney ni Muingereza
pekee mwenye rekodi nzuri.
•Iwapo Manchester City itashinda
itapunguza pengo la pointi inazozidiwa Manchester United. Lakini pia pengo hilo
litategemea na matokeo ya Manchester United na QPR, ambayo itachezwa kabla ya
mehi ya Arsenal Vs City. Kwa sasa City inazidiwa pointi tano.
•Aleksandar Kolarov amepiga krosi
16 katika nafasi za wazi mwishoni mwa wiki iliyopita ambayo ni idadi kubwa
msimu huu. Winga wa Wolves, Matt Jarvis alipiga 17 dhidi ya Newcastle Oktoba,
mwaka jana.
VIKOSI VYA LEO:
ARSENAL: Szczesny, Sagna,
Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta, Song, Rosicky, Walcott, Van Persie na
Gervinho.
MANCHESTER CITY: Hart, Zabaleta,
K Toure, Kompany, Kolarov, Barry, Y Toure, Nasri, Aguero, Balotelli na Dzeko.