Ferguson kulia na Scholes |
KOCHA Sir Alex Ferguson hana
majeruhi wapya kikosi mwake kuelekea mechi ya leo na zaidi atakuwa na nguvu mpya
ya kurejea kwa Nani, ambaye amekosa mechi tano zilizopita kwa maumivu ya
kifundo cha mguu.
Bosi huyo wa United anatarajiwa
kufanya mabadiliko kikosi mwake baada ya timu hiyo kwa sababu ya mechi tatu
katika wiki moja.
Pamoja na hayo, anatarajiwa
kumpanga winga aliye katika fomu ya juu, Antonio Valencia na hiyo maana yake Ashley Young ataanzia benchi.
Michael Owen hajapona sawasawa
kiasi cha kucheza leo Uwanja wa Old Trafford na pamoja na hayo, chaguo kuu la Sir
Alex katika safu ya ushambuliaji itakuwa ana ni kuwapanga pamoja Wayne Rooney na
Danny Welbeck au Javier Hernandez.
Mabadiliko mengine, Chris
Smalling anaweza kuchukua nafasi ya Rafael na Paul Scholes akampisha Phil
Jones.
Kocha wa QPR, Mark Hughes atamkosa
Djibril Cisse anayetumikia adhabu, ambaye atakosa mechi ya pili katika adhabu
yake ya kufungiwa mechi nne. Armand Traore na Fitz Hall bado hawatakuwapo.
Pamoja na hayo, wote DJ Campbell
na Heidar Helguson wamerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa muda.
JE WAJUA?
•Manchester United ikishinda leo
inaweza kufikisha poini nane za kuwazidi wapinzani wao katika mbio za taji la
Ligi Kuu, Manchester City, japo kwa saa kadhaa.
•Mashetani Wekundu wameshinda mechi 10 katika
mechi zao 11 zilizopita, ikishinda mechi saba mfululizo.
•Vijajna wa Sir Alex wamewafunga
QPR mara tisa katika mechi 12 zilizopita baina yan timu hizo.
•United imefungwa mechi mbili tu katika mechi
zao 36 walizocheza kwenye Uwanja wa Old Trafford, wameshinda 32.
•Vinara wa Ligi Kuu wamefungwa bao moja tu
katika mechi tano zilizopita za ligi nyumbani.
•Antonio Valencia ametoa pasi za mabao 12 na kufunga mabao manne katika mechi zake 16 alizocheza
za ligi hadi sasa.
•QPR imefungwa mechi 15 kati yas 19 zilizopita
kwenye Uwanja wa at Old Trafford,ilishineda moja tu.
•Vijana wa Hughes walibeba pointi mbili tu katika
mechi 9 zilizopita.
•Lakini wanaweza kutiwa nguvu na ushindi wao
dhidi ya Arsenal wiki iliyopita wa 2-1 kwenye Uwanja wa Loftus Road..
•Anton Ferdinand, kaka wa beki wa United, Rio,
amejifunga katika mechi mbili zilizopita alizokwenda Old Trafford.
•Rangers imeshindwa kulinda nyavu zake kuguswa
katika mechi 12 nje ya Uwanja wa nyumbani.
PROBABLE LINEUPS
MANCHESTER UNITED: De Gea, Smalling,
Ferdinand, Evans, Evra
Valencia, Jones, Carrick, Nani, Rooney
na Welbeck.
QPR: Kenny, Young, Ferdinand,
Onuoha, Taiwo, Mackie, Barton, Derry, Diakite, Taarabt na Zamora.