Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji wa Biashara wa Benki ya BPZ kutoka Zanzibar Bw. Juma Hafidhi (kushoto) akizungumza machache kwa niaba ya benki hiyo, ambapo amesema benki yao imeona umuhimu mkubwa wa kudhamini uzinduzi wa kipindi hicho kwani manufaa yake ni muhimu kwa jamii ambayo ndio wateja wao. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Palatte Media Co Ltd Bw. Redemptus Masanja na kulia ni Mmiliki wa Maduka ya Hussein Pamba Kali Bw. Hussein Maulid.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Palatte Media Co Ltd Bw. Redemptus Masanja akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa Dokumentari ya Kwanza ya
kipindi cha luninga cha "MWANA DAR ES SALAAM itakayoitwa 'SAFARI YA
NUNGWI'. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji wa Biashara wa
Benki ya BPZ kutoka Zanzibar Bw. Juma Hafidhi.
Vyombo
husika nchini vimetakiwa kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu usalama wao
wawapo safarini na jinsi ya kujiokoa pindi majanga yanapotokea iwe
majini na hata barabarani.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa
dokumentari ya kwanza ya kipindi kipya cha luninga kiitwacho ‘MWANA DAR
ES SALAAM’ Mkurugenzi wa Kampuni ya Palatte Media Co Ltd Bw. Redemptus
Masanja amesema kipindi hicho kitakuwa kikitangazwa na mtangazaji
maarufu Mussa Hussein.
Amesema
sehemu ya kwanza ya kipindi hicho imepewa jina la ‘SAFARI YA NUNGWI’ na
kuwa imekusanya taarifa mbali mbali kuhusu tukio zima la kuzama kwa
meli ya MV Spice Islander, iliyozama katika kina cha bahari cha mita 350
wakati ikitoka Unguja kuelekea kisiwani Pemba mnamo Septemba 10, 2011
na kuacha msiba kwa taifa.
Amefafanua
kuwa kipindi cha ‘MWANA DAR ES SALAAM’ kitakuwa kimebeba masuala mbali
mbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na kitafanya uchambuzi wa kina
katika matukio mbali mbali yaliyotokea au yanayoendelea kutokea nchini.
Kipindi
hicho kinachoandaliwa na kampuni ya Palatte Media Co Ltd na kutangazwa
na Mussa Hussein kitakuwa kikirushwa mara mbili kwa wiki katika luninga
ya Clouds TV siku ya Jumapili Saa 1 jioni na kurudiwa siku ya Jumanne
Saa 9 Alasiri na Ijumaa Saa 12 jioni.
Kipindi
cha televisheni cha ‘MWANA DAR ES SALAAM’ kitazinduliwa rasmi tarehe 28
April 2012 katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa ‘Dar Live’
uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Bw.
Hafidhi pia amesema PBZ katika kuonyesha inawajali wateja wake ambao
pia ni wasafiri wa kati ya Zanzibar na Dar es Salaam kila siku, benki
hiyo imefungua matawi mawili, moja likiwa katika Benki ya Kiislam ya PBZ
ambalo linapatikana katika mtaa wa Lumumba na Mahiwa na tawi jingine ni
la Conventional Bank ambalo linapatikana mtaa wa Swahili na Mkunguni.
Katika
kuhakikisha wananchi wanafurahia huduma zao, benki ya PBZ ni mwanachama
katika Mtandao wa ATM ya Umoja Switch ambao utawasaidia wateja wake
hasa wale wafanyabiashara kupata huduma ya kutoa fedha popote waendapo.
Aidha
ametoa wito kwa wafanyabiashara haswa wanaosafiri kati ya Dar es Salaam
na Zanzibar au Dar es Salaam kwenda mikoa mingine ya Tanzania kuweka
fedha zao katika matawi yao yaliyopo Dar es Salaam na kuweza kuzitoa kwa
kutumia mashine za ATM pindi wanapofika huko waendako, badala ya
kusafiri na lundo la fedha.