Na Mwandishi
wetu
WAREMBO 14 wanataraji kupanda jukwaani Mei 5 mwaka huu,
katika Ukumbi wa Wenge Garden ulipo Ukonga Mombasa, jijini Dar es Salaam kuwania
taji la Redds Miss Ukonga 2012.
Akizungumza na Blogu hii mratibu wa Shindano hilo Daudi
Mambya amesema kuwa warembo wote hao 14 wapo tayari kwa kuchuana vikali siku
hiyo na maandalizi kwaajili ya shindano hilo yanaenda vizuri.
“Warembo wote wapo kamili na tayari wako na ari kubwa ya
kushindana jumamosi hii, na hadi sasa hakuna mrembo ambaye anatatizo”, amesema
Mambya.
Aidha Mambya amesema awali warembo hao ilikuwa wachujwe
na kubaki 12 lakini kutokana na warembo wote kuwa na vigezo wameamua kuwaacha
ili kuleta ushindani zaidi siku ya mashindano.
Warembo hao ambao watapanda jukwaani kwa show kali na
yaaina yake ya ufunguzi mwaka huu katika majukwaa ya Urembo nchini wataongozwa
na Burudani kali kutoka kwa Mapacha 3.
Mbali na kundi hilo la Mapacha 3 ambalo linawika Jijini
Dar es Salaam kutokana na uhodari wao pia kutakuwepo na burudani nyingine za
wasanii wa kizazi kipya.
Mambya aliwataja warembo hao 14 watakao panda jukwaani
kuwa ni Shekha Shally, Zainab Matagi, Mageshi Boniface, Juliana Henry, Mary
Chizi, Leah John’s na Magdalena Gisse.
Wengine watakao shiriki Redds Miss Ukonga
2012 ni pamoja na Zawadi Mwambe, Stellah Maurice, Amina Sangawe, Elizabeth
Pertty, Alicia Donatus, Rachel Isaaack na Amina Ramadhani.
Shindano la Miss Ukonga 2012 linadhaminiwa na Redds
Primium Cold, Clouds FM, Father Kidevu Blog, Kiota Jungle, V Mask Logistic,
Mambya Insurance, Mamushka Pub & Catering, Hill tech Resort, Mr Mabaga, G
Obonyo na Excel Beaut Salon.