MKURUGENZI wa
Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo amesema kwamba
wachezaji wa Tanzania wanacheza tu soka bila ya kuwa ndoto, jambo ambalo
limewafanya wasifike mbali.
Akizungumza katika
hafla maalum ya kuwapongeza wachezaji wa Azam FC kwa kushika nafasi ya pili
katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Thadeo ambaye ni beki wa zamani wa
Yanga, amesema kwamba kutokuwa na ndoto kwa wachezaji wa Tanzania ni tatizo
kubwa.
Akizungumza katika
hafla hiyo iliyoandaliwa na Azam FC kwenye hoteli ya JB Belmonte katikati ya
Jiji la Dar es Salaam, Thadeo aliwataka viongozi kuchangia ndoto zao za kuwa
timu tishio Tanzania na wachezaji wao.
Alisema iwapo Azam
itakuwa na ndoto ya kufika mbali bila ya wachezaji wao na ndoto hiyo itakuwa ni
sawa na kuchukua sukari na kumwaga baharini.
“Lazima wachezaji
wa Azam wawe na ndoto ya kufika mbali, ndipo ndoto za Azam FC zitatimia kwa
urahisi,”alisema Thadeo.
Aidha, Thadeo
aliwataka Azam wasiogope mkwara wa Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage
ambaye mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, alisema Azam wacheze ligi
wakigombea nafasi ya pili tu, wakithubutu kuchukua ubingwa timu yao
itakufa.
“Katika historia,
timu zote zilizochukua ubingwa msimu uliofuata zilishuka na kufa kabisa kasoro
Mtibwa Sugar tu, hivyo nawaomba Azam wacheze ligi wakigombea nafasi ya pili tu
kila mwaka,”alisema Rage.
Basi la Azam |
Akimjibu Rage,
Thadeo alisema; “Madai kwamba mkichukua ubingwa timu yenu itakufa, ilikuwa
wakati huo, siyo sasa, hizo timu zilizokufa zilikuwa hazina misingi bora,
hazikuwa na academy, hawakuwekeza, ila Azam iko imara. Nawapongeza sana na
nawaomba endeleeni na juhudi zenu hivyo hivyo.
Pamoja na madai ya
Rage, timu zikichukua ubingwa zinakufa, lakini msimu huu mbali na Mtibwa Sugar,
mabingwa mara mbili mfululizo 1999 na 2000, msimu huu wa ligi ukiacha Simba na
Yanga, ulishirikisha bingwa mwingine wa zamani wa ligi hiyo, Coastal Union ya
Tanga waliochukua taji hilo mwaka 1988.
Timu zilizowahi
kuchukua ubingwa na sasa hazipo kwenye ramani ya soka ni Mseto mwaka 1975 na
Tukuyu Stars mwaka 1986, Pan African imeshuka tu daraja na inapigania kurejea
Ligi Kuu, ingawa haina makali ya awali na hiyo ni kama alivyoseam Thadeo
hawajawekeza.
Naye Mwenyekiti wa
Azam FC, Abubakar Bakhresa alilaani hila na njama ilizokuwa ikifanyiwa timu yake
masimu huu ili kuwadhoofisha, ikiwemo kuwapiga marefa wa mechi
zao.
Abubakar alisema
kwamba pamoja na hila hizo hawakukata tamaa, walipigana hadi dakika ya mwisho na
kufanikiwa kupata nafasi ya pili kwenye ligi, ambayo itawawezesha kushiriki
Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
“Soka Tanzania sasa
inainuka na imekuwa ajira nzuri na wachezaji wengi sasa wanavutiwa kucheza
Tanzania. Mchezaji anaona bora kuja kucheza Azam, kuliko kwenda kuhangaika
sehemu nyingine.
Wachezaji wa Azam
wanalipwa vizuri, wanaishi vizuri na wanafurahia maisha na ajira yao
nzuri,”alisema.
Alisema wakati
wanashiriki Ligi Kuu msimu wa kwanza, ndoto zao zilikuwa kucheza ili kubaki
kwenye ligi, lakini msimu wao wa nne, wanashika nafasi ya pili na hayo
wanayachukulia kama mafanikio makubwa.
Alisema mafanikio
haya ni mwendelezo wa mafanikio yaliyoanzia kwenye kutwaa Kombe la Mapinduzi
mapema mwaka huu visiwani Zanzibar mbele ya vigogo wa soka Tanzania, Simba na
Yanga.
Abubakar alisema
dhamira ya Azam msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufanya vizuri
kwenye Kombe la Shirikisho.
Uwanja wa Azam |
Akimalizia hotuba
yake, Abubakar aliwataka wachezaji wa Azam kutumia vizuri kipindi chao cha
likizo kwa kujitunza, ili warejee msimu ujao wakiwa vizuri. Akaagana kabisa na
wachezaji ambao hawatasajiliwa tena timu hiyo, akisema anawatakia maisha mema
popote waendako.
WASHINDI
WA TUZO ZA AZAM:
1) OUTSTANDING
PLAYER OF THE YEAR
Sr
Team- ABUBAKAR SALUM (SUREBOY)
Jr
Team – KELVIN FRIDAY
2)
BEST ATTITUDE IN TRAINING
Sr.Team
– LUCKSON KAKOLAKI
Jr.Team
– ISMAIL ADAM GAMBO
3)
BEST DISCIPLINED PLAYER ON /OFF THE FIELD
Sr.Team-
VAZIRI OMARI
Jr.Team
– ASSAD MUSA
4)
MOST PROMISING PLAYER
Sr.Team
– HAMIS MCHHA (Vialli)
Jr.Team
– ALLY KAIJAGE
5)
MOST INSPIRATIONAL PLAYER
Sr.Team
– AGREY MORRIS
Jr.Team
– ABDUL MGAYA
6)
MOTIVATIONAL PLAYER OF THE CLUB
Sr.Team
-IBRAHIM S CHIMWANGA(Shikanda)
Jr.Team
– REYNA ELLY & MUDHATIR YAHAYA
7)
FUNNIEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team
– ERASTO NYONI
Jr.Team
–HAMADI JUMA
8)
FITTEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team
– SAID MORADI
Jr.Team
–MOHAMMAD HUSEIN
9)
PLAYER OF THE YEAR
Sr.Team
– JOHN BOCCO
Jr
Team – JOSEPH KIMWAGA