WAREMBO 16 wanatarajiwa kupanda katika jukwaa
la ukumbi wa Equator Grill jijini Dar
es Salaam Ijumaa ya May 25 katika shindano la kumsaka
Miss Kurasini 2012.
Mkurugenzi
wa ZUM Fashion & entertainment,inayoandaa shindano hilo
Zuwena Mustapha alisema jana kwamba maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea vema na
kwamba mwaka huu wataendeleza historia ya kutoa mrembo bomba atakayetikisa hadi
ngazi ya Taifa.
Alisema mpaka sasa wameshapatikana wadhamini
14 kwa ajili ya kusaidia shindano hilo
ambalo linatarajiwa kuwa bomba, huku likiambatana na burudani kabambe.Taji la
kitongoji hicho linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma (pichani).
“Leo
napenda kuwaambia kuwa hadi sasa tunajumla ya wadhamini 14 ambao wamejitokeza
kudhamini shindano hilo,
lakini bado milango ipo wazi kwa yeyote anaependa kutuzamini na kusaidia
warembo wetu wa kurasini kupata zawadi nono na shindano kuwea zuri,”alisema
Mustapha.
Mustapha
alisema wadhamini wakuu wa shindano hilo
ni Nameems Wear wakisaidiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redds,
Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland
Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon
na Madishisha Video Production.
Aliwataja
warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa
vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma
(20),Linda Deus (20),Irene Sostheness 20),Neemadoree Sylvery(29),Edna Magige
(22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer
Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle
Gasper (19), Flaviana Maeda(22) na Sia Kimambo
(19).