HALI ndani ya uongozi wa klabu ya soka ya Yanga imeendelea kuwa mbaya baada ya wajumbe wengine wa kamati ya Utendaji Mzee Yusuf, Pascal Kihanga na
Mohammed Bhinda nao kutangaza kujiuzulu.
Yusuf na Bhinda walitangaza kuachia ngazi jana muda mfupi kabla ya kuanza
kwa mkutano wa wanachama wa klabu hiyo jana ambao mwisho wa siku uliadhimia kumg'oa madarakani mwenyekiti wao Lloyd Nchunga.
Chini ya mwenyekiti Lloyd Nchunga ambaye hivi karibuni amejikuta katika wakati mgumu kutokana na kutokubalika kwa wanachama, tayari viongiozi wengine walishabwaga manyanga akiwemo Makamu Mwenyekiti wake, Davis Mosha.
Pia wajumbe wa kamati ya Utendaji wakiwemo Seif Ahmed na Ali Mayay, huku mjumbe mwingine Theonest Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.
Aidha, kuna wajumbe wengine wa kamati mbalimbali za klabu hiyo nao walishatangaza kubwaga manyanga kwa nyakati tofauti.