Mchezaji wa Mickovila FC Richard Muya (kulia)
akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa Sparrow FC Athumani Ndimbo wakati wa
michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wiliya iliyochezwa kwenye uwanja wa
Tanganyika Packers jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Sparrows ilishinda 2-1.
Na Mwandishi Wetu.
TIMU tatu za Wilaya ya Kinondoni jumamosi
zilijitupa uwanjani katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17
yanayojulikana kama Copa Coca-Cola katika hatua ya ngazi ya wilaya , mechi hizo
zilichezwa kwenye viwanja vya Tanganyika
Peaks, Kawe, Dar es Salaam.
Mechi ya kwanza ilikuwa ni baina ya timu ya A.B.C iliyoichapa timu ya Lugalo Boys magoli
3-2 huku magoli hayo yakiingizwa
kinywani na wachezaji wake Julius Edward ambaye alifunga magoli mawili na
Joseph Jacob aliyefunga goli moja.
Timu ya A.B.C ilionekana kutawala mchezo kuanzia kipindi cha
kwanza hadi timu hizo zinakwenda mapumziko kwani timu hiyo iliweza kupata
magoli mawili katika dakika ya 10 na ya 25
huku timu ya Lugalo Boys wakiwa hawajaona kitu.
Magoli mawili ya
Lugalo Boys yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake Emmanuel Michael
na Benson Zengo dakika ya 50 na 80 huku A.B.C wakaongeza goli la tatu
lililowafanya kutoka washindi katika mechi hiyo
dakika ya 85.
Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye viwanja hivyo timu ya Sparows iliinyuka timu ya Mickovila
magoli 2-1 ambapo magoli ya timu hiyo
yaliwekwa kinywani na mshambuliaji wake Abdul Said katika dakika ya 25 na 50,
huku goli la kufutia machozi la timu ya Mickovila likifungwa na Dickson Said
dakika 43 ya mchezo huo.
Hata hivyo mechi hizo zilizochezwa katika viwanja hivyo
zilimalizika kwa mchezo wa mwisho baina ya timu ya Makumbusho na Championi.Timu
ya Makumbusho ilitoka kimasomaso kwa kuichapa Championi magoli 3-2.
Magoli ya timu ya Makumbusho yaliwekwa kinywani na wachezaji
Kassimu Bokasa aliyefunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili
cha mchezo huo huku goli la tatu likiwekwa kinywani na Omary Sudy. Hata hivyo
Champion magoli yao
mawili ambayo hayakuwawezesha kufika mbali yaliwekwa wavuni na mchezaji Hassan
Abdalah.
Mwisho