BEKI wa zamani wa kimataifa wa England, Sol Campbell
ametangaza kustaafu soka, akihitimisha miongo miwili ya uwapo wake katioka
mchezo huo.
Campbell nyota wa zamanai wa Arsenal mwenye miaka 37,
amekuwa nje ya dimba bila timu tangu alipoachwa na klabu yake ya Newcastle
United mwaka jana 2011.
Beki huyo ambaye alicheza mechi yake ya kwanza ya
kimashindano akiwa na Spurs mwaka 1992, alikiambia kituo cha televisheni cha
Sky Sports News kwamba ilikuwa "Ngumu kuondoka katika mchezo huu,
ukizingatia yeye mimi ni mwanamichezo wa juu.
"Haikuwa rahisi kwangu mimi kusema imefikia mwisho, kwa
kuwa nimekuwa ndani ya mchezo kwa muda mrefui," alisema Campbell.