Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Kinondoni, Willbroad
Mutafungwa,(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, hawapo pichani juu
ya kuanza kwa michuano ya Polisi Jamii katika wilaya hiyo michezo itakayoanza
kesho kutwa ikitanguliwa na uzinduzi utakaofanyika kesho katika uwanja wa
Polisi Osterbay, kushoto kwa Mutafungwa ni Afisa Polisi jamii tarafa ya
Kinondoni, Inspekta msaidizi wa Polisi, Mkweru N. Maswale.
Michuano ya polisi jamii kwa
wilaya ya kipolisi Kinondoni, inatarajiawa kuanza keshokutwa huku ikitanguliwa
na mchakato mzima wa uzinduzi utakaofanyika kesho katika viwanja vya polisi
Osterbay.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi, Kinondoni Willbroad Mutafungwa alisema
michuano hiyo itashirikisha vijana kutoka kata nane zinazounda wilaya ya
Kipolisi ya Kinondoni.
Alizitaja kata hizo kuwa ni
Kinondoni ,Msasani,Mikocheni,Mwananyamala,Makumbusho, Hananasif, Kijitonyama na
Makongo huku akitaja aiana ya michezo kuwa ni mpira wa miguu, kuvuta kamba na
kukimbiza kuku Mutafungwa ambaye pia ni
mwenyekiti wa maandalizi ya michezo hiyo ya polisi jamii Cup, alisema kabla ya
michezo hiyo kuanza kutakluwa na utoaji wa elimu kwa vijana amabao ni walengwea
wakuu wa michuano hiyo.
“Tunataka tuwafikie vijana
zaidi kwa kuwa wao ndiyo waathirika wa matendo mbali mbali ya kihalifu, na kwa
kutumia michezo tunataraji wengi watakuwa na shughuli za kufanya na kujiondoa
katika matendo ya uhalifu”alisema Mutafungwa.
Alisema maandalizi kwa kata
zote nane zimeshakamilika na kinachosubiriwa ni wakati ufike ili vijana waanze
kuonyesha uwezo wao katika michezo.