Mzee ibrahim Akilimali 'Abramovich'
KLABU ya soka ya Yanga kesho inatarajiwa kuendesha kisomo maalum ‘hitma’ kwa ajili ya kuwarehemu
wanachama, mashabiki, wapenzi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya
haki ambapo zoezi hilo
litafanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya jangwani na Twiga na
kuongozwa nma katibu wa baraza la wazee, Ibrahim Akilimali 'Abramovich'.
“KAma mnavyojua kila msimu
mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara unapokaribia kuanza huwa tunasoma dua ya kuwarehemu wadau mbalimbali wa
Yanga waliotangulia mbele ya haki hivyo kesho ijumaa majira ya saa sita mchana
hapa klabu tutaendesha kisomo hicho ambacho kitaongozwa na Sheikh Akilimali (Ibrahim)
hivyo tunaomba wanayanga kujitokeza kwa wingi,”alisema Sendeu.
Sendeu aliongeza kuwa baada
ya dua hiyo jioni ya leo kutakuwa na mkutano maalum utakaohusisha wenyeviti na
makatibu wa matawi yote ya Yanga ya jiji la Dar es Salaam.
Yanga ni Noma yani majaribio ya Jmosi tayari mshaanza kusoma hitma....hamna cha hitma wala nini....Mambo ya ushirikina tu...ndo hivyo sasa mmepata coach Tom amtataka akalale makaburini sasa.....Msome hitma msisome kichapi ni costant kama kutafuta kipenyo 22/7
ReplyDelete