KLABU ya soka ya Yanga imetangaza kujitoa kwenye michuano ya kombe la Tanzania ‘Urafiki’
inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Visiwani Zanzibar.
Michuano
hiyo itakayotimua vumbi kwenye Uwanja wa Amaan Visiwani humo ambapo Yanga
ilikuwa ifungue kwa kucheza na Jamhuri ya Pemba huku makamu wa kwanza wa Rais,
Maalim Seif Sharif Hamad akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kwamba
sababu ya kutoshiriki michuano hiyo ni kuhofia kuwa na majeruhi wengi ambao
watapelekea kushindwa kutetetea ubingwa wao wa michuano ya Kagame.
Alisema kama
waandaaji wa michuano hiyo wangeisogeza mbele wangeweza kushiriki, lakini kwa
kuwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kagame itawawia
vigumu.
“Tunapenda
sana kushiriki michuano ya Urafiki lakini kwa vile itakuwa karibu na Kagame
itatuwia vigumu kushiriki kwani tunaweza kujikuta tunamajeruhi wengi na matokeo
yake tukashindwa kutetea vema kombe letuy la Kagame,”alisema.