Kiungo wa Kimataifa raia wa
Rwanda,Haruna Niyonzima Fabregas amerejea jana usiku na kujiunga na Kikosi cha
Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sport Club (YANGA) katika
mazoezi yanayotarajiwa kuanza leo jioni saa kumi katika uwanja wa Kaunda Jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya
klabu www.youngafricans.co.tz
kiungo huyo amesema kuchelewa kwake kulitokana na matatizo binafsi yaliyokuwa
yamemkuta wakati akiwa nchini kwao na kusababisha kuchelewa kujiunga na Kikosi
chake.
Haruna amewataka wachezaji
wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa kutwaa kombe la Kagame katika
michuano inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu, huku Yanga ikiwa ndiyo
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Niyonzima amesema tangu
alipokuwa mapunziko alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya Klabu yake ya Yanga
hasa katika zoezi la usajiri unaoendelea na kupongeza usajili huo kutokana na
baadhi ya wachezaji anaowafahamu kusajiriwa katika kikosi hicho.
Yanga itaanza kutupa karata
yake dhidi ya Atletico ya Burundi
ambapo mechi hiyo ndiyo itakayokuwa ni pekee wakati wa ufunguzi itachezwa
katika uwanja wa Taifa,Jijini Dar es
Salaam huku Simba ikaanza kampeni siku inayofuata.
Mabingwa hao watetezi kundi lake limejumuisha
na timu za Wau Salaam ya Sudan,Altetico
ya Burundi na APR ya Rwanda.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa
BARAZA la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholous Musonye
amesema mpaka sasa mdhamini ni mmoja aliyejitosa kwenye michuano hiyo ambaye ni
Rais wa Rwanda,Paul
Kagame.
Jumla ya timu 12 zitashiriki
katika michuano hiyo ambayo itaanza Julai 14 hadi Julai 28 ambapo wawakilishi
hao watatoka katika nchi za Tanzania,Uganda,DR
Congo,Djibout,Zanzibar,Kenya,Sudan Kusini,Rwanda na Burundi.(Mwandishi wetu
Louis Sendeu)