Pichani Juu na Chini ni Wanafamilia wa Jay Dee wakipakia mizigo
tayari kuelekea kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kwa ajili ya
kukabidhi msaada.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi
kabla ya kuanza safari ya kuelekea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre.
Kiongozi wa msafara LadyJay Dee akielekea
kupanda usafiri maalum
ulioandaliwa.
Wanafamilia ndani ya basi kuelekea Maunga Cente
kituo cha watoto yatima kwa shughuli nzima ya kukabidhi
msaada.
Wanafamilia Ester Ulaya Cathbert na
Maggie wakifanya shopping katika maduka ya Kinondoni njiani kuelekea kituo cha
watoto yatima cha Maunga Centre.
Judith G. Habash a.k.a Komando Binti
Machozi Lady Jay Dee akiwasili na Familia yake katika Kituo cha kulelea watoto
yatima cha Maunga Centre kilichopo
maeneo ya Kinondoni
Hananasifu.
Wanafamilia wa Jay Dee wakishuka
kwenye basi baada ya kuwasili.
Vijana wa Familia ya Jay Dee
wakishusha msosi ulioandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya watoto yatima wa
Kituo cha Maunga Centre.
Baadhi ya zawadi zilizopekwa na Jay Dee Family
katika kituo cha kuelea watoto yatima cha Maunga
Centre.
Mwanafamilia wa Jaydee Wise Monica
Kaaya akionyesha Upendo kwa mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Maunga
Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi.
Zainabu Bakari akionyesha chumba wanacholala watoto wa kiume katika kituo
hicho.
Hiki ni chumba wa
wasichana.
Hapa ni mahali wanapotundikia
neti.
Hiki ni choo wanachotumia yatima hao
ambacho hakijaezekwa na bati.
Sehemu wanatotumia kupikia
chakula.
Mtoto Khadija Mussa akisoma Risala
kwa mgeni rasmi Komando Lady Jay Dee na Familia yake (hawapo pichani) ambapo
amezungumzia changamoto ya mahali wanapoishi haparidhishi na kuwataka wadau
kujitokeza kuwasaidia kuboresha eneo lao ikiwemo Choo, Sehemu ya kulala pamoja
na ada za twisheni kwa watoto
hao.
Wanafamilia wakisikiliza risala ya
Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia
wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo
pichani).
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka
kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady Jay Dee akikabidhi msaada
uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele, Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni
za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi
wa Kituo hicho Bi. Zainabu Bakari (kushoto)
pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Khadija
Mussa.
Jay Dee Family inawakaribisha wadau
wote watakaoguswa kutoa mchango chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na
walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada
huo.
Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto)
akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay
Dee.
Pichani Juu na Chini Wanafamilia wa
Lady Jay Dee wakipakua chakula kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya
kula pamoja na watoto yatima wa kituo cha Maunga
Centre.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre
wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee
Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika
kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga
Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi
Zainabu Bakari ambapo amezungumzia changamoto
zinazowakabili ni sehemu ya kuishi wahudumu wa kituo hicho, mishahara ya
kuwalipa wahudumu na makazi ya wahudumu wa kituo
hicho.
Bi. Zuhuru Bakari alisema kituo hicho
kinalea watoto 30 ambapo watoto 20 wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi
waliowachagua wao kutokana na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya
watoto 50.
Mwanafamilia Ester Ulaya akizungumza
kwa niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema watakuwa bega kwa bega na kituo
hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili wa kusaidia kituo hicho.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na
walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na
walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo
hicho.
Zainul
Mzige wa MO BLOG alijumuika
na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga
Centre.
Wanafamilia wa Jay Dee katika picha
ya pamoja baada ya kuhitimisha zoezi zima la kutoa msaada kwa kituo cha watoto
yatima cha Maunga Centre.