Kundi
la taarab la Tanzania One Thetre (TOT) chini ya Malkia wa Mipasho nchini,
Khadija Omari Kopa litarindima katika mikoa ya Tanga na Kanda ya Ziwa baada ya
mfungo huu mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani.
Katibu
wa TOT, Gasper Tumaini alisema, jana kwamba, ziara hiyo ambayo itatumika
kutambulisha albam za ‘Full Stop’ na ‘Mjini Chuo Kikuu’ , itaanza kwa kundi
hilo kufanya shoo ya nguvu Tanga katika kurehekea Sikukuu ya Eid El Fitr.
Tumaini
alisema, Idd pili, TOT watafunga kazi katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na
kumalizia siku ya Iddi tatu katika ukumbi wa White House mjini Muheza mkoani
Tanga.
Alisema,
baada ya kuwakonga nyoyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, Khadija Kopa na
kundi lake watainua nanga na kwenda kuishusha tena Kanda ya Ziwa, katika mikoa ya
Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara na kisha kumalizia Tabora na Singida.
Alisema,
mbali na Khadija Kopa, kundi hilo litakuwa na wanamuziki wake wa taarab,
wakiwamo Abdul Misambano, Ally Star, Mwamtama Amir ‘Mama Lao’, Mariam Khamis na
Mwasiti Suleiman.