Yanga Sc
Mafunzo SC
MABINGWA watetezi wa
Kombe la Kagame, Yanga, leo wanawakabili Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ya
robo fainali itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijiji Dar es Salaam.
Yanga iliyomaliza
nafasi ya pili katika kundi la C, itakuwa na kibarua kigumu cha kuwatupa nje ya
michuano hiyo Mafunzo kama wanataka kutinga nusu fainali.
Mechi hiyo itakayoanza
majira ya saa 10 ikitanguliwa na mechi kati URA ya Uganda na APR ya Rwanda ambao
watakumbana kuanzia majira ya saa 8.
Wakati Mafunzo wakitaka
kudhihirisha umahiri wao uliowapa wakati mgumu mabingwa wa Kenya, Tusker, Yanga
wamekamia kutinga nusu fainali.
Yanga watawakabili
Mafunzo wakitoka kuvuna ushindi wa 2-0 dhidi ya APR katika mechi ya mwisho ya
hatua ya makundi.
Mechi nyingine leo
itakuwa kati ya URA, iliyomaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi 9, baada ya
kushinda mechi zote tatu.
Kocha Mkuu wa Yanga,
Tom Saintfiet alisema juzi, kikosi chake kitapambana kushinda ili kutinga nusu
fainali ya michuano hiyo.
Alisema, kwa kiwango
kilichooneshwa na vijana wake katika mechi ya tatu dhidi ya APR, hana shaka na
uwezo wa timu yake kufika fainali.
“Licha ya kuanza vibaya
michuano hii, tuliketi chini kufanyia kazi dosari, ndio maana timu imeanza
kubadilika, sina wasiwasi na mechi ya robo fainali,” alisema.