Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu
(2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3
mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Uamuzi wa kusogeza
mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo
inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za
Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya
Tunisia tayari imeshawasili.
Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi
kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi
usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu
ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom
msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza
nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba
15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.
Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao
zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala
za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa
kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom