Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa
Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji
huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli ya
Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni
itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.